Mkuu wa mkao wa Tanga Omari Mgumba akizungumza na wadau wa mahakama pamoja na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa wiki ya  msaada wa kisheria iliyoandaliwa na mahakama kuu kanda ya Tanga.

Jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Tanga Ratifa Mansoor akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya kisheria iliyofanyika katika viwanja vya Urithi Tanga leo january 22,2023.

Na Denis Chambi,  Tanga 

Mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba amewatahadharisha wazazi , walezi na jamii kwa ujumla wanaoendelea kumalizana kienyeji  na wahalifu wa vitendo vya ukatili  wa kijinsia hasa kwa watoto akiwataka  kuachana na tabia hiyo ambapo amesema serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria  ikiwemo kuwafikisha mahakamani pale wanapobainika.

Akizungumza katika uzinduzi wa wiki ya kisheria kwa mkoa wa Tanga  Mgumba amesema kuwa zipo taarifa za baadhi ya wazazi na walezi kumalizana kienyeji  na wahalifu pale  yanapotokea matukio ya kiukatili katika jamii badala ya kuwapeleka kwenye mikono ya sheria  wanasuluhisha wenyewe hali ambayo ni kinyumr cha sheria na haki za kibinafamu.

"Tunalaani vitendo vya wazazi na walezi wanaomalizana wenyewe kwa wenyewe na wahalifu wa ukatili kwenye jamii  ,kwanza hawana mamlaka hayo na ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu kisheria pamoja na katiba ya nchi  suala hili ni kosa la kijinai kama  jinai zingine zozote  wazazi hawana mamlaka wala sheria ya kumaliza  kesi zozote wenyewe kwa wenyewe hata ikitokea baba mtu kafanya kosa dhidi ya mtoto wake bado ni mkosaji na ni mhalifu kama walivyo wahalifu wengine,  nitoe rai kwa wananchi kwamba waache kumalizana kesi za kijinai kwa ngazi za familiya  au jamii" alisema Mgumba  

"Sisi kama serikali tutaendelea kuchukua hata  stahiki kwa wahalifu wote  wanaotekeleza vitendo vya kikatili kwa watoto wetu na wanajamii wengine ,  ukatili Tanga haukubaliki na sisi tumejipanga kuendelea  kuwashughulikia wananchi wote wanaotekeleza vitendo vya kiunyanyasaji hususani kwa watoto" alisema.

Aidha Mgumba  ameitaka  mahakama ya Tanga  kuendelea kutekeleza matakwa ya kikatiba katika kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia haki kwa mujibu wa sheria akiwataka kutokujihusisha na uonevu wa aina yeyote katika kutatua migogoro ya wananchi kulingana na mashauri wanayopokea  ambayo yanahitaji msaada wa kisheria.
 
"Kwa mujibu wa katiba ibara ya 7(a)  inaitaka mahakama kutochelewesha  haki  bila sababu za msingi rai yangu kwa mahakama kutekeleza takwa hili la kikatiba tuendelee kumaliza kesi zetu kwa wakati ili kupunguza malalamiko,  lakini pia kuendelea kutoa haki bila kujali nafasi ya wahusika katika jamii" alisema

Kwa upande wake Mstahiki meya wa halmashauri ya jiji la Tanga Abdurahman  Shillow ameipongeza mahakama kanda ya Tanga kwa namna inavyoendelea kuhudumia wananchi ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali  kwa wananchi pamoja na kuwapatia msaada wa kisheria jambo ambalo limeweza kupunguza na kuondoa kwa kiasi kikubwa malalamiko  katika jamii.

"Niishukuru  sana mahakama kanda ya Tanga pamoja na watendaji wake wote   tunapongeza kwa sababu hii inatoa hamasa  na uelewa mkubwa  kwa wananchi kujua kama mahakama ipo na inahudumia jamii ambao ndio wadau wakubwa  wa shughuli zote za mahakama na tunajua kama katika usuluhishi wa migogoro ndio njia muafaka kwa sababu kunakua na uwiano   na maridhiano  baina ya pande zote  mbili tofauti wakikitumia vyema kipengele cha usuluhishi" alisema Shillow.

Akizungumza naibu msajili wa mahakama kuu Kanda ya Tanga  Beda Nyaki alibainisha kuwa bado jamii ina uelewa mdogo wa maswala ya kisheria  hivyo katika kuitumia vyema wiki hii ya msaada wa kisheria kwa kushirikiana na wadau wa mahakama wamejipanga kutoa elimu bure kwa wananchi  kupotia njia mbalimbali juu ya maswala yanayohusu sheria ili kuongeza uelewa zaidi sambamaba na kutatua migogoro iliyopo ikiwemo ukatili.

"Tafiti zinaonyesha changamoto ya wananchi wengi  wana uelewa mdogo wa maswala ya kisheria  kwahiyo tupo na wadau wetu hapa ili kusaidia  kuwapa wananchi elimu hasa juu ya madhara ya ukatili sote tunafahamu ukatili ni suala ambalo linatakiwa liwe na adhabu kali kwa wanaotekeleza makosa haya na pia kupata fidia stahiki kwa wahanga  na hilo tunaendelea kuto elimu zaidi"

Kuelekea kuanza kwa mwaka mpya wa shughuli za mahakama  kote nchini ambayo ni february mosi mahakama ya Tanga kwa kushirikiana na wafau mbalimbali wa sheria imejipanga kutoa elimu bure kwa wananchi  katika wiki hii  ya msaada wa kisheria kwa siku saba mfululizo  hii ikilenga hasa kuongeza uelewa kwa wananchi pamoja na kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Wiki ya msaada wa kisheria kwa mwaka huu wa 2023 imebebwa na kauli mbiu isemayo 'umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu,   wajibu wa mahakama na wadau.
Share To:

Post A Comment: