Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akiwakabidhi pikipiki zaidi 20 kwa moja ya kikundi ambacho kimepata mkopo wa asilimia 10 unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada akimkabidhi bajaji moja ya kikundi cha mtu  kimepatmlemavu ambacho mkopo wa asilimia 10 unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo

Na Fredy Mgunda, Iringa.


HALMASHAURI ya Manispaa ya Iringa imetoa mkopo wenye thamani ya kiasi cha shilingi millioni 328,680,000 kwa vikundi 44 kutokana na mapato ya ndani ya asilimia 10 ya madirio ya makusanyo.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mikopo hiyo Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda alisema kuwa wametoa mikopo kwa vikundi 18 vya wanawake, vikundi 15 vya vijana na vikundi 11 ya watu wenye ulemavu kwa kuzingatia uwiano wa 4:4:2.

Ngwanda alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imepanga kuanza kutoa mikopo kuanzia Milioni 20 na kwenda juu lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi wenye vikundi hivyo kuwa na tija kwenye mitaji yao.

Alisema kwa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wametoa zaidi ya bodaboda 20, Bajaji mbili na mikopo mingine mikubwa kwa ajili ya kilimo.

Ngwanda alisema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inatarajia kuanza kutoka mikopo kwa ajili ya vikundi ambavyo vinataka kuanzisha viwanda mbalimbali kwa lengo la kuifanya Manispaa hiyo kuwa ya viwanda kwa kuwa malighafi za viwanda mbalimbali zinapatika kirahisi.

Alisema kuwa vikundi hivyo hupatikana kuanzia ngazi ya mtaa,kata hadi ngazi ya Manispaa ya Iringa hivyo uhakiki wa vikundi hivyo umekuwa unafuata taratibu zote kama ambavyo serikali imeagiza.

Aidha Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwanda alisema kuwa bado kunachangamoto ya urejeshaji wa mikopo sio nzuri hivyo wanatafuta njia mbadala ya kuhakikisha vikundi vyote vinarejesha kwa wakati mikopo hiyo.

Kwa upande wao baadhi ya wanaufaika wa mikopo hiyo walisema kuwa wanaushukuru uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa unaongozwa na Meya Ibrahim Ngwanda kwa kuwakopesha wananchi mikopo ambayo haina riba kama taasisi nyingine za kifedha.

Walisema kwa kuwa wamepata mikopo mikubwa hivyo wapo tayari kurejesha mikopo kwa wakati ili kusaidia Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwakopesha wananchi wengine kwa kukuza uchumi na maendeleo ya Manispaa hiyo.


 
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: