FARIDA MANGUBE -MVOMERO, MOROGORO.

Wananchi zaidi ya 2000 wa Kata ya Lubungo na Mingo Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro  wameondokana na adha kutembea zaidi kilometa 10 kufuata maji kwenye mito na mabwawa ambayo walikuwa wakichangia wanyama wakari (Tembo) hali iliyokuwa ikitarisha maisha yao baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa Lubungo.

Hayo yameelezwa na Diwani wa Kata ya Lubungo Hamidu Zuberi kwenye ufunguzi wa Mradi wa maji wa Lubungo ulioghalimu zaidi milioni 400 fedha zilizotolewa na Mfuko wa Maji (NWF) na  kutekelezwa  na RUWASA.

 Alisema utekelezwaji wa  Mradi huo umeenda kumshusha Mama ndoo kichwani kwa sasa wananchi wachangii tena maji na Tembo kama hapo awali na kwamba wameshapoteza wapendwa wao 4 na wengine kupata ulemavu wakati wakienda kwenye mito na mabwawa.

“Nimshukuru sana Mama yetu Mhe. Dk. Samia Saluhu Hassani kwa fedha hizi za mradi wa maji kata ya Lubungo kiukweli Mama ametuheshimisha mimi pamoja na Mbunge wangu Mhe. Ze land sasa tunapita kifua mbele.” Alisema Diwani. 

Akizungumza kwenye mkutano wa adhara na wananchi wa Kata ya Lubungo Waziri wa Maji Jumaa Uweso aliwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Mvomero na Mkoa wa Mrogoro kwa ujumla kuwa Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya maji itahakikisha kila mwananchi anapata maji safi na salama.

Aidha aliwataka wananchi walio karibu na maradi wa maji kuulinda na kuutunza ili waendelee kupata huduma ya maji safi na salama kila wakati kwani serikali inatumia fedha nyingi katika kutekeleza miradi hiyo ili wananchi waweze kupata maji.

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mvomero Mhandisi Sospeter Lutonja alisema mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi CHAKWELE CO.LTD ambapo utekelezwaji wake ulianza 04.10 2018 na kukamilika rasmi 22.11.2021 na kuhudumia wananchi 2016.

Alisema  mradi umegharimu milioni 417,078,804.52 na mpaka sasa mkandarasi amelipwa kiasi cha shilingi 406,460,795.18 na tayari chombo cha watumia maji ngazi ya jamii kimeshaundwa kwa mujibu wa sheria ya maji safi na usafi wa mazingira Na. 5 ya mwaka 2019 lengo ni kuulinda mradi hu.

Utekelezaji waMaradi huo ulijumuisha ujenzi wa Tanki la maji ujazo wa 90,000, mnara wa mita 6, ununuzi na ulazaji wa mabomba umbali wa mita 4020, ujenzi wa vituo 16 vya kuchotea maji pamoja na ununuzi na ufungaji wa mitambo ya nishati ya jua 9KW.

Awali akisoma taarifa ya mradi wa Maji wa Homboza kwa Waziri Aweso Mhandisi Lutonja alisema mradi huo unatarijiwa kuwanufaisha wakazi 25,027 wa Vijiji vya Tandali, Homboza, Pekomisegese , Mlali, Kipera, umegharimu, Kinyenze, Mkuyuni, Lukuyu na Chehelo ambao umegharimu bil. 2, 945,684,663.33 bila ya VAT na mpaka kufika 5.12 2022 mkandarasi ilishalipwa 781,020,314.62.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mvomero Jonas Van Zeeland alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dk Samia Suluhu Hassani kwa kuwatua wanawake wa Jimbo hilo ndoo kichwani kwani moja ya kero kubwa ilikuwa ni maji na sasa imekwisha kabisa.



Share To:

Post A Comment: