Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi, Dikson lutevele (VILA) akiongea na wanachama wa chama hicho kata ya Mapanda juu ya umuhimu wa nidhamu ya uongozi.
Baadhi ya a wajumbe wa Halmashauri kuu ya kata ya Mapanda.

  

Na Fredy Mgunda, Iringa.CHAMA cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kimesema hakipo tayari kiwavumilia madiwani waliotumia vibaya mikopo ya vikundi ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa blog hii, katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi, Dikson lutevele (VILA) alisema kuwa lengo la serikali kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani ni kwa ajili ya kukuza mitaji ya vikundi na sio madiwani.

Lutevele alisema kuwa haiwezekani chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi kikamvumilia diwani anayezichezea fedha za Serikali ambazo zimetakiwa kupelekwa kwa vikundi kwa ajili ya kukuza mitaji ya vikundi kwa maendeleo ya wananchi wa Halmashauri husika.

Alisema kuwa hivi karibuni kumetokea kashfa kwa baadhi ya madiwani kuandikisha vikundi hewa na kupewa mikopo kutoka Halmashauri kwa manufaa ya diwani ambao sio walengwa wa mikopo hiyo na kuwakosesha fursa wananchi wenye sifa ambao walistahili kupata mikopo hiyo.

Lutevele alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kimeanza vikao kwa ajili ya kuwachukulia hatua kali madiwani wote waliobainika kuunda vikundi hewa vya mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri husika.

Alisema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi hakipo tayari kiwavumilia madiwani wote ambao wanakichafua chama kwa kuanzisha vikundi hewa na kuchukua mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri.

Lutevele alisema kuwa anampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukijenga nchi na chama kwa ujumla

Lutevele alimazia kwa kusema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi kipo kwa ajili ya kusimamia serikali na kukijenga chama hicho kutokana na ilani ya uchaguzi wa chama cha mapinduzi ya mwaka 2020/2025.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: