Katibu Wa Siasa na uenezi CCM wilayani Geita Gabriel Nyasilu,wamejikuta wakijibishana na kada wa Chama cha Mapinduzi Wilayani humo John Kishomba baada ya kada huyo kuposti picha ikionyesha stendi ya  Njombe,Mpanda na Geita  suala ambalo lilibua mjadala kwenye group la mtandao wa whatsapp la Wabunge wa Geita na kudai kitendo hicho ni sawa na kuposti vitu ambavyo havina uhalisia.

Kupitia Posti hiyo ya Stendi Katibu wa mwenezi wa CCM wilayani humo,Gabriel Nyasilu aliandika na kukiri kuwa ni kweli Stendi hiyo ina matatizo kwa sasa lakini jitihada za ukarabati zinaendelea.

“Stend yetu ina changamoto kubwa ila hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa ni hizi mara kwa mara na hizi picha ni za siku tano Nyuma  Pamoja na kutokuwa na stend Bora kama mikoa mingine lakini lazima tusifu walau hizi hatua za Dharula maana ni jitihada za viongozi wetu “Gabriel Nyasilu

Hata hivyo baada ya majibu hayo John Kishomba alimtaka Katibu wa siasa kutambua group hilo ni na lengo lake ni kueleza matatizo yaliyopo ndani ya Mkoa wa Geita na hatua ambazo wabunge wanatakiwa kuzichukua kwa kukarabati miundo mbinu.

“Hiyo akili ulitakiwa uijibu kwa fikra maana hili group sio la kusifia Ukitafakari maana ya group ni kutoa elimu, kuelimishana na kusema ukweli,Sasa unapokuja na chuki zako binafi unakosea usiwe mbwatukaji Alafu mimi na wewe hatujawahi kukaa kiti kimoja tukajenga hoja bali tumetofautiana hoja.Sasa nikusaidie cheo ulicho nacho sio cha kubwatuka”John Kishomba.

Kufuatia majibu haya yalimpelekea Katibu wa Siasa na uenezi CCM wilayani Humo ,Gabriel Nyasilu akimtaja kada huyo aache utapeli kutokana na kwamba anachokifanya ni kuuchafua mkoa na Jimbo la Geita Mjini.

“Mimi na wewe wote kwa sasa tuna TIN NUMBER jitahidi ujue hatua kadhaa nilizonazo itakusaidia acha kukariri  Naweza kuwa unavyofikiria ila mimi sio Tapeli kama wewe “Gabriel Nyasilu.

 Kufuatia majibu haya Kada huyo wa CCM ambaye ni mmiliki wa Kampuni ya udalali ya Jolas Investiment alimtaka katibu huyo kutengua kauli ya kumuita Tapeli kutokana na kudai kuwa na familia pamoja na watoto ambao wanamtegemea huku akinukuu vifungu vya katiba ya chama ambavyo kiongozi anatakiwa kuvifuata.

“Timiza majukumu yako ya CCM ,Achana na mambo ya kipuuzi utambue cheo ulichonacho ukitumikie vyema na kwa uadilifu, Kwa mujibu wa katiba ya chama cha mapinduzi timiza majukumu;Katibu wa siasa na uenezi wa wilaya ibara ya 84 sura ya 83 kifungu a hadi f;

Kushughulika masuala yote ya itikadi,Siasa na Sera za CCM katika Wilaya. Kupanga na kusimamia mafunzo na maandalizi ya makada na wanachama katika Wilaya.Kufuatiria utekelezaji wa Sera za chama za kijamii na ilani ya uchaguzi ya CCM katika Wilaya. Kudumisha uhusiano mzuri na vyombo vya habari na kuwa na mipango ya mawasiliano na uhamasishaji wa umma kwa ujumla katika Wilaya. Kufuatiria hari ya kisiasa na harakati za vyama vya kisiasa wilayani . Kufuatia mwenendo wa jumuiya za kijamii katika Wilaya.

Hata hivyo mjadala na majibishano hayo yalifungwa baada ya ndugu John Kishomba kuweka muongozo wa Katiba ya Chama cha CCM juu ya Majukumu ya Katibu wa Siasa na uenezi wa CCM.


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: