Na Tiganya Vincent-Mahakama -Katavi

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania , Mhe. Mustapher Mohamed Siyani atakuwa Mgeni Rasmi katika hafla za uzinduzi wa majengo matatu (3) ya Mahakama za Hakimu Mkazi tarehe 18 Januari 2023.

Uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi.Majengo yatakayozinduliwa siku hiyo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi, Lindi na Songwe ambayo yamejengwa kwa kutumia fedha za ndani na nimwendelezo wa uzinduzi wa miradi ya majengo ya Mahakama yanayozinduliwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini. 

Kukamilika kwa ujenzi wa miradi hiyo katika mikoa tofauti hapa nchini umezingatia mahitaji ya kisasa kwa wadau wa mnyororo wa utoaji haki ambapo kuna ofisi za Mawakili, Maafisa Magereza, Ustawi wa Jamii, maeneo kwa ajili ya Watu wenye mahitaji maalum na watoto wamewekewa vyumba vya kutumia wakiwa mahakamani.

Kuzinduliwa kwa majengo hayo katika Mikoa hiyo mitatu kutaongeza ufanisi na utoaji huduma kwa wananchi kwani majengo haya yana mazingira rafiki ya utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kutumia mfumo ya kitekinolojia ya habari na mawasiliano.

Share To:

Post A Comment: