Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wafugaji wa wilaya hiyo juu ya uingizwaji holela wa mifugo
Baadhi ya viongozi wa wafugaji wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa

Na Fredy Mgunda, Iringa.



SERIKALI Wilaya ya Iringa imepiga marufuku uingizwaji holela wa mifugo Wilayani humo na kuahidi kuanzisha oparesheni maalum ya kijiji kwa kijiji kuhakiki mifugo iliyyopo na kuwaondosha wafugaji waliovamia kutoka nje ya wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amesema yapo madai kuwa baadhi ya viongozi wa serikali za vijiji amekuwa na tabia ya kuwapokea kiholela wafugaji kutoka maeneo mbambali ikiwamo wanaoondoshwa katika bonde la usangu wilayani Mbarali katika opareshen maalum ya kunusuru ikolojia ya Ruaha inayoharibiwa na shughuli za ufugaji holelela katika Eneo Hilo unaosababisha kupungua Kwa maji katika mto Ruaha na kuhatarisha uhaibwa wanyamapori na mazingira.

Moyo alisema Serikali haiko Tayari kuwafumbia macho viongozinwa namna hiyo wanaokiuka miiko ya uongozi na kwamba viongozi watakaobainika kuruhu mifugo kuingiza kiholela katika vijiji vyao watawajibishwa kwa mujibu wa Sheria kwani kwa kiwango kikubwa wamekuwa wakichochea ongezeko la migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa Ardhi wakiwemo wakulima.

Mkuu wa Wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati aya ulinzi na usalama Wilayani humo aliyasema hayo wakati wa mkutano baina ya kamati hiyo na Wafugaji wa Asili mkutano uliolenga kujadiliana namna ya kuboresha shughuli za ufugaji Kwa na kuondosha migogoro iliyopo wilayani humo

Kiongozi hiyo kupitia Risala ya Wafugaji alipokea malalamiko ya kadhaa ikiwemo Vitendo vya urasiku vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa vijiji ikiwemo kupora maeneo yaliyotengwa Kwa shughuli za ufugaji na kuyabadikishia matumizi Hali inayopelekea Wafugaji kukosa maeneo ya malisho na kulazimika kulisha katika maeneo yasiyo rasmi, Hali inayoibua migogoro ya mara Kwa mara

Aidha Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wafugaji Wilaya ya Iringa vijijini Emmanuel Sailutye alizitaja changamoto nyingine ni 
Suala la Wizara ya mifugo kutokuwa na sera ya kutambua maeneo yaliyotengwa Kwa ajili ya Wafugaji, Kutozwa fedha kiholele Kwa makosa ya kuingia katika maeneo yasiyoruhusiwa pamoja na Upanuzi wa mipaka ya hifadhi na kuanzishwa Kwa hifadhi ya jamii Mbomipa hatua inayopelekea Wafugaji kukosa maeneo ya malisho

Kufuatia malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alimuagiza Mkuu wa Idara ya Ardhi Wilayani humo kuwasilisha taarifa ya mpango wa matumizi Bora ya Ardhi wa Kila Kijiji Ili Serikali iweze kuchukua hatua endapo wapo viongozi waliobadili matumizi ya maeneo hayo kinyume na taratibu, Huku akiwataka Wafugaji kuwa watulivu wakati Kamati ya ulinzi ikiendelea kushughulikia malalamiko na maombi yaliyotolewa na Wafugaji hao.

Wakati wa mkutano huo Mjumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Iringa Kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Iringa Anneth Mwakatobe licha ya kusisitiza utulivu Kwa Wafugaji na wanachi Kwa ujumla pia aliwasihi kujiepusha na Vitendo vya Rushwa Huku akiwataka kutoa Taarifa kwa Taasisi hiyo pindi wanapoombwa Rushwa na viongozi pamoja na watu wanaowarubuni kuwa watawasaidia pindi wanapokumbana na Changamoto katika shughuli zao.

Afisa hiyo kutoka Ofisi ya TAKUKURU alisema Serikali Iko macho kushughulikia changamoto zote zinazoikabili wananchi wake hivyo utoaji wa Rushwa ama upokeaji wa Rushwa ni ukiukwaji wa mikakati ya utoaji huduma Kwa wananchi

Mwakatobe liitaja Namba ya TAKUKURU ambayo ni 144 akiwahimiza wananchi kuitunia Namba hiyo kutoa Taarifa za Siri pindi wanapoombwa Rushwa ama wanaposhughulia dalili za Rushwa katika maeneo ya mbalimbali akisiisitiza kuwa Rushwa ni Adui wa Haki.


Mwisho

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: