Na Denis Chambi, Tanga.

HALMASHAURI ya wilaya ya Bumbuli imekuwa kinara kati ya halmashauri zote 11 zilizopo ndani ya mkoa wa Tanga ikiongoza katika zoezi la uandikishaji wa wanafunzi wa shule za awali na msingi kwa muhula mpya wa masomo 2023 ikifikisha asilimia 68 kwenye zoezi hilo ambalo bado linaendelea  hadi January 30 mwaka huu. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na zoezi hilo mkuu wa mkoa wa Tanga Omari Mgumba amesema kuwa lengo la mkoa huo kwa ujumla kwa muhula mpya wa masomo 2023 ilikuwa ni kufikia asilimia 100 ya uandikishaji lakini hadi sasa ni wanafunzi 52708 (elfu hamsini na mbili mia saba na nane) wamekwisha kuandikishwa kati sitini na mbili mia tano hamsini na nne ( 62554) katika ngazi za awali na msingi zoezi ambalo lilianza November 2022 hadi January 24,2023 sawa na asilimia 84.3 . 

"Elimu ya awali ni msingi mzuri sana kwa wanafunzi wanapoanza elimu ya msingi uandikishaji wa wanafunzi kwa ngazi ya awali na shule za msingi ulianza tangu mwei November 2022 hadi kufikia january 24, 2023 siku ya elimu duniani wanafunzi walioandikishwa katika ngazi ya awali ndani ya mkoa wa Tanga ni elfu hasini na mbili mia saba na nane kati ya elfu sitini na mbili mia tano hamsini na nne ambao tumetarajia kuwaandikisha hiyo ni sawa na asilimia 84.3 ikiwa ni wavulana 29532 na wasichana 26176 mkoa na wilaya unaendelea na zoezi la uansikishaji ili kufikia lengo la asilimia 100 kama tulivyotarajia "

 "Na katika hili niwapongeze sana halmashauri ya Bumbuli ndio imekuwa halmashauri ya kwanza kutimiza watoto wa shule ya awali kutimiza watoto wa ngazi ya awali  asilimia 114.6 wakifwatiwa na Handeni ni ambao asilimia 108 na halmashauri ya mwisho ni Tanga jiji ina asilimia 78.5" alisema Mgumba

 "Uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi kufikia janury 24 , 2023 jumla ya wanafunzi elfu sitini na tano mia nne sitini na moja (65, 461) kati ya wanafunzi elfu sabini mia sita themanini na sita (7686) wanaotarajia kuandikishwa sawa na asilimia sitini na mbili wameandikishwa kuanza darasa la kwanza kwa mwaka mpya wa masomo" 

"Na katika hili pia ni halmashauri ya Bumbuli ndio wameongoza ina asilimia 112 ya pili tena ni Handeni mjini ina asilimia 107 na ya mwisho ni Korogwe vijijini ina ailimia 74.9 jumla ya halmashauri zote 11 ndio tunafikia asilimia 92.6 ni imani yangu mpaka january 30 kwa mkoa wa Tanga tutakuwatumefikia asilimia 100. 

Aidha Mgumba amebainisha kuwa katika shule za sekondari kwa mkoa mzima wa Tanga wanafunzi walioripoti na kuanza masomo ni elfu thelasini na tano mia tisa arobani na nane (35948) kati ya wanafunzi elfu hamsini mia sita kumi na nne (50, 614)  wamesharipoti mashuleni na kusajiliwa ni sawa na asilimia 76.18 ambapo wavulana ni 18688 na wasichana 19962 walishasajiliwa kidato cha kwanza mwaka 2023 . 

"Walioripoti kwenye shule zetu za mkoa wa Tanga kwa kidato cha kwanza jumla ya wanafunzi hadi kufikia january 24,2023 jumla ya wanafunzi elfu 35 mia tisa arobaini na nane kati ya wanafunzi elfu hamsini mia sita kumi na nne wameshafika mashuleni na kusajiliwa ikiwa wavulana ni  18688 na wasichana ni  19962 sawa na asilimia 76.18  na katika kundi hili pia waliofanya vizuri ni Korogwe mjini na halamashauri iliyofwatia ni Pangani na ya mwisho ni kilindi. 

Hata hivyo mkuu wa mkoa amewaasa wazazi walezi na jamii kwa ujumla kutambua umuhimu wa elimu wakihamasika kuwapeleka watoto wao mashuleni kuhakikisha kuwa watoto wote walio na umri wa kuwepo shuleni hawabaki nyumbani huku akiwataka kutambu kuwa bado wanamchango mkubwa wa kusaidiana na serikali kukuza sekta ya elimu hapa nchini.
Share To:

Post A Comment: