Mkurugenzi wa taasisi  isiyo ya kiserikali ya Tree of Hope  jiji la  Tanga Fortunata Manyeresa.

Na Denis Chambi, Tanga.

MSTAHIKI  meya wa halmashauri ya jiji la Tanga Abdurahman Shillow amewataka madiwani kwa kushirikiana watendaji , wakuu wa idara na wenyeviti wa mitaa kutoka kata zote 27 za jiji hilo kushirikiana kwa pamoja katika kuendelea kupiga vita vitendo vya ukatili pamoja na kuhakikisha shuguli zote za kijamii zinazofanyika katika maeneo yao haziathiri maadili kwa watoto. 

Shillow ametoa wito huo wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha viongozi hao kufanya tathmni ya mradi wa kupinga ukatili kwa watoto na vijana balehe uliokuwa ukitekelezwa taasisi za Tree of Hope pamoja na Tanga Youth Tallent Association (TAYOTA) kwa ufadhili wa shirika la Botner foundation uliotekelezwa kwa miezi 6. 

"Ki ukweli hali ya Tanga ni mbaya sio nzuri sana naomba twendeni tukaangalie wanaojihusisha  na mapenzi ya jinsia moja , wanaoishi kwenye mitaa yetu lakini tuangalie vigodoro sheria yetu inasema shuguli ama sherehe zote mwisho ni saa sita usiku  lakini wazazi wahakikishe watoto wenye umri wa miaka 18 hawaendi kwenye maeneo ya starehe ni maeneo ambayo ni hatarishi kwa sababu ndiko vinakofanyika vitendo vya hovyo" alisema Shillow.

 "Huu ni mmomonyoko wa maadili kwa sababu sasa hivi watanzania tumebeba tamaduni za kigeni na zina madhara makubwa mno madiwani wenzangu tuvae viatu vya uhusika kwenye jamii niwaombe sana mshirikiane na wenyeviti wa mitaa muwatambue tusaidiane sisi kama viongozi tuone tunasimamia nafasi zetu vipi " alisema Shillow. 

Amesema suala la mkoa wa Tanga kutajwa kuongoza kukithiri kwa vitendo vya ukatili , matumizi ya madawa ya kulevya , ni matukio ambayo hayakubaliki na yanapaswa kuendelea kupigwa vita kuazia ngazi za familia viongozi wa serikali taasisi na wadau mbalimbali wa maendeleo kila mmoja kutumia nafasi yake kukemea pamoja na kutoa taarifa katika mamlaka husika ili sheria ziweze kuchukuliwa. 

"Suala la mkoa wa Tanga kutajwa kuongoza katika maswala ukatili wa kijinsia , matumizi ya madawa ya kulevya, na mengineyo ukiangalia na jiographia ya mji wa Tanga jinsi tulivyo ni kwamba tumeathirika sana matendo haya hakubaliki , sasa kila mtu kwa nafasi yake aone madhara ya matendo haya waswahili wanasema 'mwana mleavyo ndivyo akuavyo" alisema . 

Aidhamstahiki meya  amewapongeza taasisi ya Tree of hope pamoja na Tanga Youth Tallent Association kwa namna walivyotekeleza mradi huo wenye lengo la kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto pamoja na kundi balehe ambapo amewataka kuendeleza mpango huo wa kutoa elimu kwa jamii kuanzia ngazi za mitaa ili malengo yaweze kufikiwa 

"Mpango wa kupinga vitendo vya ukatili katika jamii ni suala ambalo litachukuwa muda mrefu sana wa kuwabadilisha watu na tabia zao, watumieni sana wenyeviti wa mitaa na madiwani hawa ndio wenye watu ili tuweze kupata matokeo yenye uhalisia kwa urahisi" 

Awali akizungumza mkurugenzi wa taasisi ya Tree of Hope Fortunata Manyeresa alisema licha ya jitihada zinazoendelea kutokomeza ukatili kwenye jamii bado hali sio nzuri sana kutokana na vitendo hivyo kukithiri kila kukicha hivyo kuwaomba wadau mbalimbali na  viongozi wa serikali kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha sheria kali zinachukuliwa dhidi ya wale wote wanaotekeleza na kuwaathiri watoto ambao ni Taifa la kesho.

 Alisema katika kipindi chote cha kutekeleza mradi huo wamefanikiwa kuunda kamati mbalimbali za MTAKUWA kuwafikia wanafunzi elfu 16 , kuunda klabu mbalimbali za wanafunzi katika shule za msingi na sekondari hii ikiwa ni jitihada za kuendelea kupiga vita na kupiga vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto katika jamii. 

"Ki   ukweli bado  maswala ya ukatili wa kijinsia yanatuumiza kila kukicha, tumeunda kamati za mtakuwa katika kata zote 27 tumeweza kuwafikia wanafunzi elfu 16 kwa mujibu wa ripoti yetu tuna klabu kwenye shule zote za msingi na sekondari  zilizopo jiji la Tanga na tutaendelea kuzijengea uwezo kadiri nafasi itakavyotokea, lakini pia tumewafikia madaktari dawati la jinsia , waendesha mashtaka ili kuhakikisha haki inatendeka " alisema Manyeresa. 

Kwa upande wake afisa maendeleo wa jiji la Tanga Simon Mdende kwa niaba ya mkurugenzi . wa halmashauri hiyo amewapongeza TAYOTA pamoja na Tree of Hope kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kupiga vita ukatili wa kijinsia katika jamii hapa nchini.
Share To:

Post A Comment: