Na Denis Chambi, Tanga.

Meneja wa timu ya Misitu FC Juma Salum amesema kuwa wamejipanga kutwaa kombe la ligi ya mkoa wa Tanga ' TRFA' na katika kuonyesha kuwa wana nia ya dhati kabisa tayari wameshatenga bajeti ya kanda ambako watakwenda kuungana na mabingwa wa mikoa mingine kuchuana kuelekea kutafuta tiketi ya kucheza ligi darajala pili msimu ujao. 

 Timu hiyo amabayo inaiwakilisha wilaya ya Lushoto leo jumatano itashuka dimbani kucheza mchezo wake wa nusu fainali dhidi ya bingwa mtetezi wa ligi hiyo vijana na Middle Age Veterans mchezo utakaochezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani ambapo mshidi atakwenda fainali kupepetana na timu  itakayoshinda kati ya Watumishi  FC au Eagle ili kumtafuta bingwa wa msimu huu. 

 Akizungumza meneja huyo amesema kuwa wanataka kuweka historia kwa wilaya ya Lushoto ambayo tangu kuanza kwa ligi hiyo haijawahi kutwaa taji la mkoa na sasa wanakwemda kufuta uteja huo na kuwaonyesha wadau na wapenda soka kuwa sasa wilaya hiyo imefunguka kimichezo na sio kama enzi hizo. 

 Salum alisema  kuwa haikuwa rahisi mpaka wao kufika hatua hiyo kutokana na msimu huu kusheheni vipaji kutoka kwa wachezaji mbalimbali kwa timu pinzani   lakini malengo waliyojiwekea kama timu wakishirikiana na chama cha soka wilaya ya Lushoto  kutaka kutwaa ubingwa huo ndiyo yanayowafanya mpaka sasa wawe na shauku kubwa ya kuta ka kulitimiza jambo lao.

 "Sisi matarajio yetu ni kuchukuwa ubingwa na kujivisha jukumu la mkoa kwenda kuutetea kwaajili ya kupanda ngazi  kanda , ligi daraja la pili na mbeleni pia, kwa kutambua hilo tupo vizuri kiuchumi tumeshajipanga na mpaka sasa tumeahajiwekea bajeti ya kanda niwaahidi tu wana tanga mara baada ya kufanikiwa kuchukuwa ubingwa kwajinsi tulivyojipanga naamini tutakuwa na timu ligi daraja la pili msimu ujao" 

 "Kupitia chama cha soka cha wilaya ya Lushoto tuliweza kukaa kikao cha ushirikiano ili kuweza kupelekea ubingwa mkoa , wapenzi na mashabiki wetu wameipokea timu vizuri na wameamka kupitia timu ya Misitu siku ya tarehe 28 kwenye mchezo wetu wa nusu fainali uwanjani patakuwa hapatoshi, kuna gari zaidi ya 20 ambazo zitabeba mashabiki  kutoka Lushoto kuja kuishangilia timu" 

 Hii unaweza ukasema ni vita ya patashika nguo kuchanika kati wilaya ya Lushoto na Tanga kwani ndizo pekee zilizofanikiwa kuingiza timu zote mbili ambapo Tanga inawakilishwa na Eagle FC pamoja na Veterans Middle Age huku Lushoto ikiwakilishwa na Misitu FC pamoja na Watumishi FC.
Share To:

Post A Comment: