Rais wa Shirikisho la Sanaa za Maonesho Tanzania Bi. Synthia Henjewele akimkabidhi Balozi wa Airtel Tanzania Lucas Mhuvile almaarufu Joti Tuzo Filamu Bora - Ucheshi (Best Comedy) kupitia Tuzo za Filamu Tanzania 2022 zilizofanyika Disemba 17, 2022 Ukumbi wa Mikutano wa  Kimataifa  wa AICC jijini Arusha.
...................................................
.
Na Mwandishi Wetu, Arusha.

KAMPUNI ya Airtel Tanzania inayotoa huduma za mawasiliano ya simu imekuwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua Sekta ya Filamu naMichezo ya Kuigiza nchini ambapo ilikuwa moja ya Makampuni yaliyodhamini Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania linaloratibiwa na Serikali kupitia Taasisi yake ya Bodi ya Filamu Tanzania.

Kilele cha Tamasha la Tuzo za Filamu Tanzania 2022 kimefanyika Tarehe 17 Disemba, 2022 jijini Arusha katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha - AICC,ni Tamasha la pili kuratibiwa na Serikali kupitia Bodi ya Filamu, ambapo limetoa jumla ya washindi wa Tuzo 32 kutoka katika Filamu 59 zilizofanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro. Aidha, Tamasha la kwanza lilifanyika mwaka 2021 jijini Mbeya.

Akizungumza katika usiku wa kilele hicho Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia alikuwa mgeni rasmi alisisitiza kuwa,dhamira ya Serikali ni kuendelea kuwekeza katika kuwasaidia Wasanii ili waweze kufanya vizuri, ambapo tayari Serikali imeanzisha Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao utaanza kutoa mikopo kwa Wasanii kuanzia jumatano ya Disemba 21, 2022.

“Sekta ya Filamu inakua, na inaendelea kutoa ajira kwa vijana wengi pamoja na kuchangia katika Pato la Taifa, hivyo sisi kama Serikali tutaendelea kuweka nguvukatika Sekta hiyo" amesema Mhe. Mchengerwa.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo alisema nia ya Serikali ya kuanzisha Programu hii ya kutunuku wadau wake Tuzo ni:

 “kutambua mchango wa wanatasnia ya Filamu,b. kutambua vipaji vilivyojificha vya wanatasnia ya Filamu,c. kuongeza hamasa kwa wanatasnia ya kuzalisha kazi nyingi zaidi za Filamu,d. kuongeza hamasa kwa wanatasnia ya Filamu kuzalisha kazi bora za Filamuna hatimaye kuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya nchi, nae. kusisimua fursa za uwekezaji katika Sekta ya Filamu nchini”.

Aidha, kupitia zoezi hili zima la Tamasha la Tuzo hapa nchini, Serikali itapata Taswira itakayoweza kusaidia kuandaa program maalumu za kuwajengea uwezo watendaji wetu wa filamu kulingana na mahitaji yao halisi.

Kampuni ya Airtel Tanzania ilikuwa moja ya Makampuni yaliyodhamini Tamasha laTuzo za Filamu 2022 na iliwakilishwa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Bi. MonicaErnest ambapo alipata nafasi ya kukabidhi Tuzo ya Filamu bora - Mapambo Atharikwa mshindi wa kipengele hicho Bw. Jafari Athumani kupitia Filamu ya Mateka.

Aidha, Meneja huyo alisema kuwa Kampuni ya Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia Sekta za Sanaa hususani Filamu, ambapo imeanzisha Televisheni Mtandao (Airtel Tv) yenye lengo la kusaidia Wasanii wa Filamu nchini kuuza kazi zao kupitia mtandao huo, ambapo wasanii hao wanapata fedha kutokana na wingi wa watazamaji ndani na nje ya nchini hivyo kuongeza pato la Wasanii mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kupitia kodi.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: