Na John Walter-Manyara.

Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara wamesheherekea miaka sita tangu Hifadhi ya Mlima Hanang ipandishwe hadhi.

Mkuu wa wilaya ya Hanang Janeth Mayanja ameongoza sherehe hizo zilizohudhuriwa pia na wakazi wengi wilayani hapo. 

Mayanja amesema idadi ya watu wanaoupanda Mlima Hanang ambao ni wa nne kwa urefu Tanzania inaongezeka kila siku kwa sababu Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha ambazo zimeboresha miundombinu katika hifadhi ya mlima huo kunzia geti la kuingilia, vyoo vya kisasa na njia za kuelekea juu ya mlima. 

Amewataka wakazi wa Hanang, Tanzania na nje ya nchi kutenga muda na kupanda mlima huo wenye sifa nyingi za kuvutia ikiwemo mandhari nzuri.

Hifadhi ya mazingira asilia ya Mlima Hanang ilipandishwa hadhi kuwa hifadhi ya Taifa Novemba 11,2016. 

Amesema changamoto zizilizopo ni watu kuingiza mifugoi kwenye hifadhi, uchomaji moto msitu, uvamizi wa hifadhi kwa matumizi mbalimbali ya binadamu. 

Urefu wa mita 3,423 kutoa usawa wa bahari na ndo mlima mrefu zaidi kwa kanda ya kati. 

Kwa mwaka 2022 January hadi Novemba 11, watalii zaidi ya 1,500 wametembelea hifadhi hiyo iiyoko mkoani Manyara kaskazini mwa Tanzania. 

Afisa masoko wa hifadhi asilia ya Mlima Hanang’ Elizabeth Mbunda amesema katika hifadhi hiyo kuna maporomoko ya maji,msitu mnene, hali ya hewa nzuri huku akivitaja viingilio ni shilingi 2,000 tu kwa Watanzania. 

Kingine cha kuvutia ni utalii wa ibada maalum za maombi zinazofanywa na Wabarbaig ndani ya msitu huo.
Share To:

Post A Comment: