Afisa Uhusiano wa Tanga UWASA Devotha Mayala  akizungumza wakati  wa kutambulisha mradi wa Maji Safi Kijiji cha Madanga wilayani Pangani katika mkutano na wananchi wa eneo hilo kuutambulisha mradi wa uboreshaji wa upatikanaji wa maji kutokana na kijiji hicho kuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji muda mrefu .

 

Afisa Uhusiano wa Tanga UWASA Devotha Mayala  akizungumza wakati  wa kutambulisha mradi wa Maji Safi Kijiji cha Madanga wilayani Pangani katika mkutano na wananchi wa eneo hilo kuutambulisha mradi wa uboreshaji wa upatikanaji wa maji kutokana na kijiji hicho kuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji muda mrefu .

Meneja wa Tanga Uwasa wilaya ya Pangani John Fussi akizungumza wakati wa mkutano huo

 Msimamizi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Safi Kijiji cha Madanga kutoka Tanga Uwasa Abubakari Mtili akielezea mradi huo
Na Oscar Assenga, PANGANI.


Zaidi ya Milioni 480 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya mradi wa uboreshaji wa maji safi katika Kijiji cha Madanga, Kimang'a mpaka Jaira wilayani Pangani ili kuweza kuondosha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji iliyopo eneo hilo.


Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Maji Safi Kijiji cha Madanga kutoka Tanga Uwasa Abubakari Mtili wakati wa mkutano na wananchi wa eneo hilo kuutambulisha mradi wa uboreshaji wa upatikanaji wa maji kutokana na kijiji hicho kuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji muda mrefu .


Alisema kutokana na uwepo wa changamoto hiyo Wizara ilifikiria kuchimba visima katika maeneo hayo ili kuongeza upatikanaji wa maji lakini havikuwa na maji ya kutosha hivyo wao wamejipanga kuchukua maji katika eneo la Boza.


Alisema hivyo wao kama Tanga UWASA wamejipanga kuchukua maji katika eneo la Boza ambapo kuna visima watachimba kwa kuongeza na vilivyopo ili kuhakikisha huduma hiyo inapatikana na kuweza kuondoa tatizo la maji.


" Ndugu zangu leo tumefika hapa kuutambilisha mradi na kuwaomba muwe tayari kuupokea ili tuweze kuondosha changamoto ya maji lakini pia tunaomba ushirikiano wenu" Alisema


Aidha alisema kwamba katika utekelezaji wa mradi huo wanatumia vibarua kutoka kwenye eneo hilo na hivyo wananchi watapata ajira ya kuchimba mitaro na kazi nyengine ndogondogo katika utekelezaji wa mradi huo.


Alisema katika utekelezaji wa mradi huo hawajachukua mkandarasi ili kuhakikisha wanashiriki moja kwa moja wao wana mafundi wamewapa mkataba wa kufanya kazi za ufundi kwa hiyo kupitia wao wanatoa ajira kwa vijana waliopo maeneo hayo ambao watakuwa wapo tayari.


" Tanga UWASA imejipanga kuanza utekelezaji wa uboreshaji wa miundombinu wa Maji Safi katika eneo la Madanga mpaka Jaira kama mnavyofahamu kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji muda mrefu" Alisema.


"Hivyo tumeanzisha mradi kuhakikisha maji yanafika kwenye maeneo yao, maji yatatoka kwenye chanzo kilichopo eneo la Boza na kusafirisha maji hayo mpaka kwenye tenki lililopo eneo la Jaira na maji hayo yataenda kwa wananchi na wananchi wataruhusiwa kuunganishiwa maji mpaka nyumbani" Alisema


Hata hivyo alisema mradi wa Madanga na Kimang'a ulikuwa na changamoto ya maji muda mrefu ila kupitia mradi huo wananchi watapata maji ya kutosha kutokana na mradi huo ambapo pisi 2,500 za mabomba zimeshafika kwa ajili ya kutekeleza mradi huo na wanatarajia wananchi wa eneo hilo watanufaika .


Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Afisa Uhusiano wa Tanga UWASA Devotha Mayala alisema mradi huo utasaidia kupunguza kero ya maji kwa wananchi huku akiwataka wawe mabalozi wa kuhakikisha wanautunza na kuulinda.


Alisema kwa sasa Tanga UWASA inatoa huduma maeneo matatu kwa mkoa wa Tanga ambapo ni Pangani, Muheza na Tanga Jiji na wamefika eneo Jaira kwa lengo kuongea na wananchi kuhusu mradi ambao watautekeleza kuboresha huduma ya maji kwa wananchi.


Alisema kwamba kimsingi walipewa eneo la Pangani tokea mwaka 2019 na tokea walipopewa wameweza kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji mpaka kufikia asilimia 70 na katika kuhakikisha wanafanikisha huduma ya maji maeneo wanayoyahudumia wanatekeleza miradi mbalimbali ya uboreshaji.


Alisema miradi hiyo ni kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji na kukarabati miundombinu iliyokuwa chakavu kuhakikisha watu wanapata maji kwa muda wote, kwa Pangani wanatakeleza mradi wa Madanga - Kimang'a ambao lengo kubwa kuongeza huduma ya maji kwa wakazi wa pembezoni maana sasa huduma inapatikana kwa wingi eneo la mjini.


Alisema kwamba mradi huo utalenga maeneo ya pembezoni Madanga, Kimang'a na Jaira, pia alisema sio kwamba wanatekeleza mradi Pangani pekee kwa mfano Tanga katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa sasa wana mradi miundombinu wa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji awamu ya pili ambao kwa sasa unaendelea hatua za ukingoni ulianza mwaka Jana Agosti na wanatarajia mwishoni mwa mwaka huu utakuwa umeshakamilika na kukamilika kwake kutafanikisha upatikanaji maji ya uhakika kwa wakazi wa Tanga jiji na Muheza.


Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha barabara ya Pangani, ndugu Haji Mohamed alisema wameupokea mradi huo wa Tanga UWASA kwa mikono miwili kutokana na kwamba Kijiji chao cha Madanga kina changamoto kubwa ya maji na hivyo wanategemea kupata maji kutoka kwenye taasisi za dini kuwasaidia.


Alisema wanawakaribisha Tanga UWASa waje wasimamie vizuri mradi huo ili waweze kuondokana na changamoto hiyo ya upatikanaji wa huduma ya maji.


"Tunawakaribisha Tanga UWASA kwani tunajua wana uwezo mkubwa wa kusimamia miradi hivyo tunaamini watautekeleza kwa waledi mkubwa na hivyo kuwa na tija" Alisema.


Mwisho
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: