•SASA IMEBAKIA WIKI MOJA , Tiketi nane ( 8 ) na vifurushi sita ( 6 ) vya vifaa vya nyumbani kutoka Hisense kutolewa.


 Baadhi ya washindi wa safari ya kwenda QATAR kushuhudia kombe la dunia , Promosheni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na HISENSE wiki ya Sita katika picha ya pamoja .


Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutta ( kushoto ) akikabidhi mfano wa tiketi kwa mmoja wa washindi wa Safari ya kwenda QATAR promosheni ya WAKISHUA TWENZETU Qatar na HISENSE Wiki ya sita.Afisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE Bwn. Joseph Mavura ( kulia ) akikabidhi  vifaa vya ndani kutoka Kampeni ya Hisense kwa baadhi ya washindi wa Promosheni ya Wakishua Twenzetu QATAR na HISENSE wiki ya sita , vifaa hivyo ni Tv inchi 50 , Friji , Microwave na Subwoofer . Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutta.

..................................................#####################..........................................................

Ijumaa ya Novemba 11, 2022, Kampuni inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wameendelea kutoa  tiketi za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia na zawadi ya Vyombo vya ndani kama vile Friji , Spika za mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave, sasa imebaki wiki moja ya promosheni hii na Jumla ya washindi nane ( 8 ) wa tiketi , na washindi sita ( 6 ) wa Vifaa vya Hisense wanahitajika ndani ya wiki hii moja. 

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema kuwa;

“Washindi wa leo wamepatikana kwenye Droo ya wiki ya sita ya promotion yetu ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense  washindi hawa walifanya miamala mbalimbali ikiwemo kulipa bili, kufanya malipo ya serikali, kupokea pesa kutoka nchi za nje, Banki, mitandao mingine, Lipa kwa simu, kununua muda wa maongezi,kuchukua mikopo kupitia tigo pesa na huduma nyingine za Tigo pesa na baada ya kufanya hivyo waliingia kwenye droo na baadaye kuibuka washindi wa kampeni ya WAKISHUA TWENZETU QUATAR NA HISENSE, Kwa wateja wetu wa Tigo endeleeni kufanya miamala na Tigo pesa ili kuibuka washindi, Hadi sasa imebaki wiki moja na ndani ya wiki hii moja tunawatafuta washindi 8 watakao kwenda kushuhudia kombe la dunia mubashara (LIVE) na washindi 6 wengine watajipatia kifurushi cha vifaa vya ndani vya kampuni ya hisense. 

Ikumbukwe kuwa washindi wetu wa Safari ya kwenda kushuhudia kombe la Dunia Qatar, safari yenu iliyolipiwa kila kitu itaanzia Airport Jijini Dar Es Salaam hadi Dubai ambapo mtalala hapo na kesho yake safari ya Qatar kuangalia mechi na baadaye mtarudi Dubai kutalii na kuangalia mazingira kabla ya kurejea nchini " Alimalizia.

Naye Afisa masoko wa kampuni ya HISENSE Bwn.Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense

Inatoa punguzo la 20% katika maduka yao yote na huduma ya kusafirishiwa bidhaa utakazo nunua hadi nyumbani kwako bure (FREEE DELIVERY), hii ni kwa wateja wote watakao nunua bidhaa kutoka hisense na kulipia kwa njia ya Tigo pesa. Alimalizia

Bi. Diana Morshidu Abbas miaka 26 Mfanyakazi wa ndani Jijini Dar Es Salaam  na Bwn.Aggrey Enock Muongi mwanafunzi wa mwaka wa nne sheria katika chuo cha UDSM ni miongoni mwa baadhi ya washindi wa vifaa vya ndani vya kampuni ya Hisense ambavyo ni Tv yenye ukubwa wa inchi 50, Friji, Microwave na Subwoofer wameeleza namna walivyofurahia baada ya kukabidhiwa vifaa vya ndani kutoka kampuni ya Hisense ikiwa ni baada ya kufanya miamala ya Tigo Pesa  

“Nilipo pigiwa simu na namba 100 ya Tigo kuambiwa kuwa nimeibuka mshindi wa vifaa vya ndani vya kampuni ya Hisense sikuamini kwasababu matapeli wamekuwa ni wengi siku hizi,Hivyo baada ya kupewa maelekezo kuwa natakiwa kufika makao makuu ya Tigo ili niweze kujipatia zawadi zangu Ndipo nilipoamini kuwa ni kweli nimeibuka kuwa mshindi , vifaa hivi kweli vitalibadilisha geto langu na litakua kivutio kikubwa , si hivyo tu bali Tigo na Hisense wamenipa mwanzo mzuri wa maisha hasa pale ntakapomaliza masomo yangu , niwaombe watanzania wenzangu tusiipuuzie hii kampeni ya wakishua ni ya kweli kabisa , unachotakiwa ni kufanya miamala kwa wingi zawadi bado zipo wenda ukaibuka kuwa mshindi ukajipatia vifaaa vya ndani au ukasafiri kwenda Qatar kushuhudia mechi ya kombe la Dunia mubashara” Alisema Bwn. Aggrey

Naye Mmoja wa washindi wa Tiketi ya kwenda Qatar kushuhudia kombe la dunia Bwn. Khalid Shimiyu akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa mfano wa tiketi ya ndege amesema kuwa

" kwakweli Tigo na Hisense wametimiza ndoto yangu , kuna kipindi kombe la dunia lilifanyika Afrika Kusini nlitamani sana niende ila kutokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wangu ikiwemo za kiuchumi nlishindwa kabisa kwenda , lakini sasa ona kwa kufanya miamala ya Tigo Pesa tu napelekwa kushuhudia BURE kabisa maana nshalipiwa kila kitu kuanzia usafiri ,maradhi na hela ya kujikimu , asanteni sana Tigo "

Ikumbukwe hii ni wiki ya sita tangu promosheni hii itangazwe hawa ni baadhi ya walioibuka kidedea kwa kuwa washindi wa safari ya kuelekea Qatar  kushuhudia kombe la dunia ambao ni Qatar Zahra Fayaz Nasser, Hemedi Abdallah Mohamed , Neema Kisha Patrick, Mohammed Issa Walele, Kitaja Thomas Mwankosole, Khalidi Bufungile Shimiyu na Ahmed Salim Kijuu,  wamejishindia nafasi ya kwenda kushuhudia kombe la dunia huko nchini Qatar kupitia miamala ya Tigo Pesa.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: