• Wateja kupata intaneti ya GB 78 bila malipo kwa mwaka mzima

Dar es Salaam. Tarehe 15 Novemba, 2022. Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali nchini Tanzania, Tigo Tanzania, imeshirikiana na kampuni ya Samsung kuzindua mfululizo wa simu janja za Samsung A04 nchini Tanzania. Ushirikiano huo ni sehemu ya harakati za kampuni ya Tigo kuongeza matumizi ya mtandao nchini kupitia intaneti yake 4G na kukuza teknolojia.

Meneja wa Bidhaa za Intaneti Bi. Imelda Edward akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu za kisasa za Samsung A04 alisema, 

“Tigo bado inashirikiana tena na Samsung Tanzania kuwaletea simu bora na za uhakika, Pamoja na maendeleo yaliyopatikana katika kuboresha utumiaji wa simu janja, bado kuna nafasi ya kuboreshwa na ndiyo maana, tunaendelea kuwekeza katika ubia unaolenga kutoa matokeo yanayotarajiwa ya kupenya kwa karibu 100% katika siku za usoni na ndio maana leo hii tunawaletea toleo jipya la mfululizo wa AO4 Nchini Tanzania , Wateja watafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wetu wa kasi zaidi wa 4G ambao ni mkubwa zaidi nchini. 

Baada ya kununua Samsung A04 na A04s tunatoa data ya intaneti ya GB 78 BURE kwa mwaka mzima kwa wateja wote nchini kote, karibuni sana katika maduka yetu ya Tigo na Samsung mjipatie ofa hizi na simu hizi kwa bei nafuu kabisa ". Alimalizia Bi. Imelda

Kwa upande mwingine , Mkuu wa Kitengo cha biashara Samsung Tanzania, Mgope Kiwanga alisema, “Toleo la Samsung Galaxy A04 limejaa vipengele vya kupendeza ambavyo vitapeleka maisha yako kwenye kiwango kipya Kwanza ina skrini nzuri ya inchi sita na kamera ya megapixel 50, ambayo ina uwezo mkubwa wa kuchukua matukio mbalimbali ya picha na video kwa kiwango cha hali ya juu. Betri nzuri ya kudumu itahakikisha kuwa unakaa mtandaoni na kuwasiliana kwa muda mrefu zaidi.Pata Galaxy A04 yako leo.

Matoleo ya simu mahiri za Samsung A04 zinapatikana katika maduka yote ya Samsung na Tigo nchini kote. Samsung A04 (64GB) itauzwa kwa 350,000 Tshs na A04s (64GB) kwa 400,000 Tshs. & A04s (128GB) kwa Tshs 450,000. & pia zitakua na waranti ya Miezi 24 kutoka Samsung.

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: