MKUU wa Wilaya ya Ngorongoro,Raymond Mwangwalla amewaagiza Wakala wa Barabaraza Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani hapo  kujenga mitaro ya kupitisha maji ili kuzuia maji hayo kutoharibu barabara nyakati za mvua.

Mangwalla alitoa maagizo hayo leo Novemba 9, 2022 wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa barabara za Tarura ndani ya mji mdogo wa Loliondo wilayani Ngorongoro kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama.

Amesema barabara nyingi zinazojengwa wilayani hapo haziwekwi mitaro ya kuzuia maji huku baadhi ya maeneo mitaro hiyo imeelekezwa katika maeneo ya watu.

Aidha, aliagiza vifusi vinavyomwagwa pembezoni mwa barabara visambazwe ili kuondoa kero kwa wananachi na vyombo vya usafiri vinavyotumia barabara hizo kabla ya mvua hazijanyesha
Share To:

Post A Comment: