Na John Walter- Babati

RAIS Samia Suluhu Hassan amezindua barabara za Mitaa za Mji wa Babati kilometa 8.1 na kuahidi kujenga bararaba za lami umbali wa kilometa tano katika Mji huo.

Amezindua barabara hiyo leo Novemba 22,2022 na kutoa ahadi hiyo mara baada ya uzinduzi.

Amesema serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya barabara ili kusaidia wananchi kufanya shughuli zao.

Vile vile alizindua vihenge na maghala ya kuhifadhia mazao ambavyo vimejengwa Mjini Babati ili kulinda usalama wa chakula.

Naye waziri wa kilimo Hussein Bashe amemshukuru Rais kwa kuzindua vihenge hivyo na aliahidi kuwa hadi kufikia mwaka ujao serikali inataka iwe ina uwezo wa kuhifadhi tani 500,000 Nchi nzima.

Akitoa taarifa ya mradi  huo Ofisa mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula (NFRA) Milton Lupa amesema kukamilika kwa mradi huo katika eneo la Babati kumeongeza uwezo wa kuhifadhi nafaka kufikia tani 79,000 kwa Kanda ya Arusha ambayo inajumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro  na Manyara.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa Babati  wameishukru serikali kwa kujenga vihenge hivyo na kuzindua barabara ambayo imewaondolea vumbi katika mji wa Babati.

Share To:

Post A Comment: