Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekabidhi vifaa mbalimbali vya mazoezi ya viungo kwa watoto wenye ulemavu wanaoishi pembezoni mwa Pori la Akiba la Pande ikiwa ni sehemu ya tamasha la kuhamasisha utalii wa ndani.


Tamasha hilo limefanyika Novemba 19,2022 lilihusisha utalii wa michezo ya mbio za baiskeli na mbio za kukimbia kwa miguu katika Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaam, Na Walioshinda Mbio za Baiskeli Km33 ni King Amani Matambuu na Queen Jamila Abdula na Kwa upande wa Km21 ni King Edson Mwakalukwa na Queen Aneth Dankan Wote Hawa Watafanya kazi ya Kutangaza Utalii katika Pori la Akiba la Pande. 


"Washiriki wote waliokimbia mbio za baiskeli kilomita 33, Mbio za kukimbia kwa miguu kilomita 21,10, na 5 kiingilio kilichotoka kimeweza kuchangia upatikanaji wa vifaa vya hawa watoto wenye ulemavu" Pia katika Shughuli hii Wamepatiakana Ma Queen Wawili na Ma King Wawili wa Pori la Pande ambao kwa Pamoja wametunukiwa Taji la Ubalozi wa TAWA kwa Muda wa Mwaka Mmoja Mpaka Tamasha Lingine La Mwakani, Wote hawa watafanya kazi ya kutangaza Utalii ndani katika Pori la Akiba la Pande na watafanya kazi kwa karibu na TAWA.


Hata Hivyo Mwenyekiti wa Board ya TAWA amesisitiza burudani na shamrashamra hizo zitaendelea kwa kuwa na mpango wa kuanzisha TAWA weekend Bash! Ambapo kila mwisho wa #Week tutakuwa tunakutana Pori la Pande kula, kunywa na kucheza muziki huku tukitizama wanyama wanaotarajiwa kuongezwa Katika Pori la Pande. 


Aidha, Amewahamasisha watanzania wengine wenye uzalendo kuendelea kujitokeza kuchangia kundi hilo la watoto wenye ulemavu na Kusema matamasha Haya yataendelea kufanyika katika maeneo mengine ya hifadhi ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii nchini pamoja na kufungua fursa za uwekezaji


Share To:

Post A Comment: