SHAHIDI Hawa Mwaifunga ambaye ni mleta maombi namba 11 katika kesi iliyofunguliwa na wabunge wa viti maalumu 19 wa Chadema wakipinga kufukuzwa ndani ya chama hicho, ameieleza Mahakama Kuu, Masjala Kuu kuwa katika kikao kilichopelekea wao kufukuzwa uanachama alipewa nafasi ya kuomba msamaha tu na siyo kusema chochote.

Hawa amedai hayo leo Novemba 3,2022 mbele ya Jaji, Cyprian Mkeha wa Mahakama hiyo wakati

Alipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kuhojiwa na wakili wa wajibu maombi Peter Kibatala.

Amedai yeye na wenzake 18 waliitwa kuudhuria kikao cha Baraza Kuu la Chadema Mei 11 mwaka 2022 ambapo katika kikao hicho walitakiwa kuthibitisha rufaa zao.

Alidai baada ya hapo nafasi nyingine waliyopewa ni ya kuomba msamaha kabla wajumbe wa baraza hilo kupiga kura na kufikia uamuzi wa kutangaza kuwavua uanachama wao.

Hata hivyo, kabla ya kujibu hayo kulitokea mabishano huku shahidi huyo akikataa kujibu swali, baada ya kuulizwa kama alipewa nafasi ya kusema chochote katika kikao Cha baraza hilo kabla ya uamuzi wa kufukuzwa.

Shahidi huyo na wakili Kibatala walijikuta wakiingia kwenye mabishano hayo kuhusu ajenda za kikao cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika tarehe 11 Mei, 2022 kufuatia kuulizwa swali kama alipewa nafasi ya kusema chochote katika kikao hicho.

Hawa alikataa kujibu kwa kunukuu ajenda za Baraza hilo na kujibu kulingana na hati yake ya kiapo, akidai nafasi aliyopewa ni ya kuomba msamaha na si kusema chochote.

Wakili Kibatala alimuuliza shahidi kama ni kweli ama si kweli minutes zinaonesha alipewa nafasi ya kusema chochote baada ya katibu mkuu kuwasilisha taarifa Kwa niaba ya Kamati Kuu kabla ya wajumbe kupiga kura.

Shahidi Hawa amedai alipewa tu nafasi ya kuomba msamaha kabla ya wajumbe kupiga kura.

Hata hivyo wakili Kibatala alimtaka shahidi kujibu swali lake hilo ndipo Hawa akadai Kibatala anamlazimisha kusema anachotaka..." Mimi sikupewa nafasi ya kusema chochote nilipewa nafasi ya ku- apologize." Akadai Hawa

Jaji: Kwa namna hiyo hamtakaa muelewane, lazima tusonge mbele. Msimamo wako (Kibatala ) walipewa nafasi ya kusema chochote kabla ya uamuzi kutolewa. Yeye (Hawa) msimamo wake hawakupewa chochote kilichotokea ni kupewa nafasi ya ku- apologize.

Kibatala: Wala Sina msimamo, namuuliza kwa mujibu wa minutes na sio msimamo wangu, ni kweli nafasi hiyo ilitolewa?

Shahidi: Kwa mujibu wa kiapo changu, nafasi iliyotolewa kwangu ni ku-apologize.

Kutokana na mvutano huo, Jaji Mkeha alimtaka Shahidi ajibu swali kama anavyoulizwa Kwa kuwa mawakili wake watapata nafasi ya kumuuliza maswali ya ufafanuzi.

Jaji Mkeha aliwahoji Kwa nini wanakuwa wagomvi, ambapo Hawa alidai Wakili Kibatala alimpania.

Jaji: Leo mbona mnakuwa wagomvi sana?

Shahidi: Wakili amenipania

Jaji: Na wewe umempania pia?

Shahidi: Na Mimi nikampania.

Aidha, Hawa amesema, hawezi kuthibitisha kama Naibu msajili wa vyama vya siasa nchini, Sisty Nyahoza aliomba kuwepo katika kikao cha baraza kuu la chadema ili kiangalia uwazi wa upigaji kura na kuwa katika kiapo chake hakueleza kama Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, John Mnyika walikuwepo katika kikao cha Baraza kiu kilochowafukuza uanachama kwasababu katiba ya chama hicho inaeleza wanaoongoza vikao vya kufanya maamuzi
Share To:

Post A Comment: