Mahakama ya hakimu Mkazi Njombe imewahukumia miaka 10 jela Focus lutengano na Aizack Lutengano baada ya kuwakuta na hatia ya kujaribu kumua mama yao mdogo Rehema Ngimbudzi mkazi wa kijiji cha mtwango wilayani Njombe kwa kumpiga na nyundo kichwani.

Akisoma hukumu hiyo katika kikao cha mashauri ya mauaji ambacho kimefanyika mahakama ya mwanzo Makambako Hakimu mkazi mkuu mwenye mamlaka ya ziada Liadi Chamshama amesema washtakiwa hao walitenda kosa hilo septemba 21, 2016.

Licha ya adhabu ya kutumikia miaka kumi jela, wametakiwa kumlipa Mama yao mdogo Rehema ngimbudzi kila mmoja fedha kiasi cha shilingi milioni tano.

Hakimu Chamshama amesema kutoka na vitendo vya mauaji ambavyo vinaripotiwa kwa wingi mkoani Njombe mahakama hiyo inatoa adhabu hiyo ya kifungo cha miaka 10 ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Aidha Hakimu huyo wakati akisoma maelezo ya washtakiwa hao aliamuru mzamini wa mshtakiwa namba moja Christopher Joseph Salingwa kulipa faini ya shilingi milioni 4 au kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kushindwa kumfikisha mshatakiwa mahakamani,ambapo shahidi huyo amelipa faini hiyo.

Awali mawakili wa washtakiwa hao, Happy ilomo wakili wa mshtakiwa namba mbili Focus Lutengano na wakili Brighton kaguo wakili wa mstakiwa namba moja Aizack lutengano waliomba mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu kwani wanategemewa na familia na ni mara yao ya kwanza kutenda kosa hilo.

Wakili wa serikali Andrew Mandwa alimtaka hakimu kutoa adhabu  kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

Share To:

Post A Comment: