Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peter Ndomba (wa tatu kulia) akikabidhi
mtungi wa gesi kwa mmoja ya wanawake wajazito wa Kata ya Rubanda kwa niaba ya
wanawake wengine wajawazito wa wilaya ya Serengeti.Wa pili kulia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akishuhudia utolewaji wa mitungi
hiyo ya gesi kwa wanawake wajawazito wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (watatu kulia) akipokea mtungi wa gesi kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Oryx Peter Ndomba(wan ne kushoto).Tukio hilo limefanyika jana eneo la Rubanda wilayani Serengeti mkoani Mara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti iliyoratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation ambayo imejikita katika kusaidia mtoto njiti na lengo la mitungi hiyo ni kuwawezesha wanawake kutumia nishati safi ya kupikia.
Meneja Masoko wa Kampuni Peter Ndomba(kulia) akipokea cheti cha shukrani
kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel wakati wa Maadhimisho ya Siku
ya Mtoto Njiti.Cheti hicho kimeandaliwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation
ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa wadau hao katka kusaidia taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel (kushoto aliyejifunga mgolole) akizungumza umuhimu wa
kutumia nishati safi ya kupikia baada ya Kampuni ya ORYX Energies kukabidhi
mitungi ya gesi na majiko yake kwa wanawake wajawazito wilayani Serengeti
kupitia Taasisi ya Doris Mollel Foundation.
Doris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation
akisoma jina la mmoja wa wadau walioshiriki kufanikisha Siku ya Mtoto Njiti
Duniani wakati wa maadhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika wilayani Serengeti
mkoani Mara.
Viongozi wakiwa meza kuu.
Muonekano wa mitungi ya gesi kabla ya kukabidhiwa.
Na Mwandishi Wetu, Serengeti.
KAMPUNI ya Oryx Energies imekabidhi mitungi ya gesi 200 pamoja na majiko
yake kwa kwa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojishughulisha kusaidia
watoto njiti pamoja na malezi ya watoto hao ambapo mitungi hiyo imetolewa kwa
wanawake wajawazito katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kuwaondolea adha ya
kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.
Mitungi hiyo ya gesi ikiwa na majiko yake imekabidhiwa leo Novemba 20 mwaka
2022 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani ilyofanyika Kata Rubanda
wilayani Serengeti mkoani Mara na kuhudhuriwa na wananchi pamoja na viongozi wa
Serikali akiwemo Naibu Waziri wa Afya Dk.Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani.
Uamuzi wa kampuni hiyo kutoa mitungi hiyo umepongezwa na viongozi
mbalimbali walioshiriki maadhimisho hayo ambao wameeleza kitendo cha mama
mjamzito kupewa mtungi wa gesi na jiko lake inakwenda kutoa nafasi mama kulea
familia na hasa watoto na kuondokana na adha ya kwenda kukata kuni kwa ajili ya
kupikia.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Marry Masanja amesema Oryx imeona
umuhimu wa kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti kwa kutoa
mitungii ya gesi na hiyo inakwenda kusaidia kutunza mazingira na wamekuwa mfano
wa kuigwa kwani ndio kampuni ya mwanzo kabisa kuja na nishati safi ya kupikia.
“Tunawapongeza kwa jitihada zao za kuhakikisha jamii yetu inakuwa na
nishati safi ya kupikia ambayo pia inasaidia katika kutunza mazingira.Kutumia
nishati safi ya kupikia inasaidia katika
jitihada za Wizara ya Maliasili na Utaliii kulinda na kutunza mazingira,
takwimu zinaonesha asilimia 90 ya nishati isiyo safi yaani mkaa na kuni ndio
inayotumika kwenye kupikia,”amesema.
Aidha ametoa ombi kwa wadau wanaohusika na kampuni za nishati safi za
kupikia kuangalia namna ya kuifanya nishati hiyo kupatikana kwa bei nafuu
ambayo kila mwananchi anaweza kumudu kununua jiko la gesi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dk .Godwin Mollel pamoja na
kuzungumzia hatua zinazochukuliwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu
Hassan katika kuboresha afya ya mama na mtoto ikiwemo afya ya Mtoto Njiti pia
anatoa pongezi kwa Taasisi ya Doriss Mollel katika kuokoa maisha ya Watoto
Njiti na kuendelea kutoa kila aina ya misaada inayogusa jamii ya watoto njiti.
“Rais siku zote amekuwa akionesha njia lakini kwenye vifo vya mama na mtoto
ni eneo ambalo linamgusa sana .Hata kwenye hotuba yake ya kwanza bungeni
alionesha msisitizo mkubwa.Katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani
Rais wetu ameweka fedha kwenye akaunti ya Doris Mollel Foundation Sh.milioni
20.Pia Rais ametoa Sh.milioni 50 kwa ajili ya kununuliwa vifaa kwa ajili ya
Watoto Njiti.Kupitia bajeti ya mwaka huu Serikali imetenga fedha kwa ajili ya
kujengwa vituo 100 vitakavyohusika na matibabu ya watoto njiti.
“Aidha nampongeza Dorris Mollel kwa mchango wake wa kusaidia jamii hasa
watoto njiti, amekuwa hafanyi semina wala makongamano lakini kila anapoonekana
anagusa jamii moja moja.Lakini leo hapa tumeshuhudia mitungi ya gesi 200
inakabidhiwa kwa wamama wajawazito.”Nishati safi ya kupikia inakwenda kupunguza
uharibifu wa mazingira na tunafahamu mabadiliko ya kimazingira yanachangia
uwepo wa Watoto njiti.”
Awali Meneja Masoko wa Kampuni ya ORYX Energies Peter Ndomba aliyemwakilisha Mkurugenzi wa
kampuni hiyo, amesema wao wameamua kuonesha njia kwa kuamua kutoa mitungi ya
gesi kwa ajili ya kumuwezesha wamama wajawazito kuwa na nishati safi ya
kupikia.
“Tangu tulipoingia Tanzania mwaka
1999 moja ya ajenda yetu kuu ni kutetea mazingira kwa kuhakikisha jamii inakuwa
na nishati safi ya kupikia lakini pili kuimarisha afya ya watanzania hususani ya Mama ambaye
amekuwa mstari wa mbele katika familia kwa upande wa mapishi , na Doris Mollel
Foundatuion alipotuomba mitungi ya gesi hatukusita kumpatia kwasababu sisi
tulimuona mama moja kwa moja., hivyo tuliamua kushiriki bila kusita.
Aidha amesema mitungi ambayo wameitoa kwa wanawake wajawazito ni sehemu ya
kuunga mkono jitihada za Serikali ya
Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia
Suluhu Hassan inayohamasisha Watanzania kutumia zaidi nishati safi ya kupikia
badala ya kuendelea kukata kuni ambayo imekuwa ikichangia kuharibu mazingira.
Kwa upande wake wa Doris Mollel ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dorris
Mollel Foundation ameishukuru kampuni ya ORYX
kwa kumpatia mitungi hiyo ambayo aliiomba kwa ajili ya kuwasaidia
wanawake wajawazito ambao ndio wamekuwa wakihangaika kutafuta kuni kwa ajili ya
kupikia, hivyo kupatikana kwa mitungi hiyo kunakwenda kumuondolea mama mjazito
changamoto ya kutafuta kuni.
“Wakati wa mjadala wa nishati safi ya kupikia ambao ulihudhuriwa na Rais
Samia Suluhu Hassan , ndo siku ambayo nilikutana na Mkurugenzi wa Oryx ambaye
alishiriki mjadala huo na hivyo nilitumia nafasi hiyo kumuomba mitungi ya gesi
na majiko yake ili nikawapatie wanawake wajawazito.Nashukuru leo nakabidhi
mitungi hii na ndoto yangu imetimia ya kuona tunatafuta ufumbuzi wa kumuondolea
adha mama mjamzito ya kwenda mbali kutafuta kuni.”
Aidha ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wengine waljochangia vifaa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto njiti lakini kwa upekee anatoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amempatia Sh.milioni 20 kufanikisha maadhimisho hayo pamoja na Sh.milioni 50 kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali
Post A Comment: