Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Jerry Muro amemuelekeza Mkuu wa TAKUKURU Wilaya hapo kuanza uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watumishi watatu waliokuwa wanasimamia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Irisya tarafa ya Sepuka jimbo la singida magharibi

Pamoja na hatua hiyo pia amemuelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Mhe. Justice Lawrance kupeleka team ya uchunguzi ambayo itakuwa na lengo la kuchunguzi mienendo ya tabia za watumishi hao watatu ili pia waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi za halmashauri 

Dc Muro amesema hatua hiyo imekuja baada ya mradi huo kukwama mara mbili kumalizika uku kiasi cha shilingi milioni 500 kikiwa kimeshatumika chote pasipo mradi kukamilika hatua iliyosababisha mradi kukwama kumalizika kwa miezi mitatu zaidi 

Dc Muro amesema walivyofika kwa nje unaweza kuona kazi imeisha ila ukiingia ndani utabaini maabara haijakamilika, vyoo vyote vya majengo yote havijakamilika, tiles za chini hazijakamilika, jengo la mochwari ndani halijakamilika, vyoo havijafungwa vyote na masinki ya kunawia mikono hayajakamilika, uku baadhi ya majengo yakiwa tayari na nyufa kitu ambacho hakiweza kufumbiwa macho

Katika hatua ingine ya kushangaza ni kitendo cha wasimamizi wa mradi huo kuita fundi ambae alitengeneza kipande cha ngazi za kupandia jengo la  mama na mtoto na kisha kutoweka uku wakijua kuna ziara ya mkuu wa wilaya na walipoulizwa iweje walete fundi siku moja kabla na kwanini fundi huyo leo hakuwepo viongozi wote walikana kumuita na kumtambua fundi huyo uku wakijua kuna kazi imefanywa kwa siku moja tu 

Dc Muro pia ametoa maagizo ya kukamilika kwa vituo vyote vya afya ambavyo vinajengwa na hela zikiwa zote zimeshatumika na kusisitiza wasimamizi wa vituo vya afya vya Iyumbu, Ntuntu na iglanson kuwa tayari kwa lolote lile 

"Wananchi hawataki kusikia malumbano yenu kwenye ujenzi wao wanataka kuona hela zilizotolewa na Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan zinatumika ipasavyo na miradi inamalizika pasipo visingizio " ameongeza Muro.Share To:

Post A Comment: