Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17,2022 Jijini Dar es Salaam

************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka watu wote wanajihusisha na kazi za Sanaa kuhakikisha wana vibali hai vya BASATA ifikapo tarehe 30 Novemba 2021 ili kuondoa usumbufu ambao utajitokeza.

Wito huo umetolewa leo Novemba 17,2022 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dkt. Kedmon Mapana wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema mtu yeyote ambaye hatokuwa na kibali hai cha kujihusisha na shughuli ya Sanaa atachukuliwa hatua za Kisheria kama ilivyobainishwa hapo juu.

Hata hivyo amesema ni kosa kwa msanii ama mdau yeyote kujihusisha na shughuli ya Sanaa pasipo na kibali hai cha BASATA na ndapo itathibitika mtu yeyote ametenda kosa hilo Sheria na Kanuni zake imeweka adhabu ya faini ya papo kwa hapo isiyopungua milioni tatu (3,000,000), Kufungiwa kujishughulisha na kazi za Sanaa kwa kippindi kisichopungua miezi sita au zaidi na Kufutiwa usajili.

"Baraza linawasisitiza kuzingatia matakwa ya Sheria, Kanuni na Taratibu za usajili na vibali ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu zitakazotumika katika kupanga mikakati ya maendeleo ya Sekta ya Sanaa nchini". Amesema Dkt.Mapana

Aidha amesema kwa sasa Baraza linaendelea na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu usajili kupitia mfumo wa usajili mtandaoni unaotambulika kwa jina “Artist Management Information System”(AMIS) na unapatikana kwa kiungo (link) ya: www.sanaa.go.tz, watu wote wanasisitizwa kutumia mfumo huo kujisajili na kupata vibali.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: