Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Wiki ya AZAKI inayotarajiwa kuanza rasmi Oktoba 24 hadi 28, 2022 Jijini Arusha. (kushoto) ni, Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Norwegian Church Aid (NCA) Berte Marie Ulveseter, na (kulia) ni, Doreen Dominic Mkuu wa kitengo cha sekta ya umma Benki ya Stanbic.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga akifurahia jambo alipokuwa akitolea ufafanuzi moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kwenye mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za FCS Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa (FCS) Francis Kiwanga
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Norwegian Church Aid (NCA) Berte Marie Ulveseter akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (CFC) Francis Kiwanga (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa shirika la NCA Better Marie Ulveseter (kushoto), na Mkuu wa kitengo Cha sekta ya umma Benki ya Stanbic Doreen Dominic wakisikiliza maswali ya waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mkuano huo.


Imeelezwa kuwa jumla ya asasi za Kiraia (AZAKI) 500 zinakusudiwa kuhudhuria katika wiki ya AZAKi iliyopangwa kufanyika kwa siku tano kuanzia Oktoba 24 hadi 28 katika Ukumbi wa Mikutano wa Arusha (AICC) Jijini Arusha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS), Francis Kiwanga asema tukio hilo la wiki moja ni tukio muhimu kwa wadau wa maendeleo na Sekta Binafsi kujadiliana kwa pamoja katika kuleta maendeleo ya watu na taifa kwa ujumla.

Aidha ameongeza kuwa Wiki ya AZAKi inaelekeza juhudi zake katika kuhakikisha ushirikishwaji bora wa watendaji kutoka sekta mbalimbali hapa nchini.

“Kongamano hili litafanyika mkoani Arusha kwa muda wa siku tano na litakuwa la tofauti na miaka iliyopita kwa sababu tutakuwa na washiriki kutoka katika makundi tofauti, wapo washiriki ambao wametoka katika mashirika ya ndani na mashirika ya kimataifa na ushiriki mkubwa sana kutoka mashirika binafsi,”

”Wiki hii inawaleta pamoja wadau wakuu wa maendeleo na inalenga kuimarisha mahusiano na ushirikiano unaolenga kuimarisha ushiriki wa asasi za kiraia katika maendeleo ya Tanzania, kuunda jumuiya mpya na kuimarisha jumuiya zilizopo zenye lengo la kutatua changamoto kuu za maendeleo na kubadilishana mawazo”.amesema Kiwanga.

Kiwanga ameongeza kuwa asasi za kiraia znafanya kazi kwa karibu na watu na jamii kwa ujumla kupitia utekelezaji wa afua zinazosaidia uendelezaji wa usawa wa kijinsia, ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu, demokrasia, ushiriki wa vijana, amani na mshikamano wa kijamii.

‘’Sekta ya asasi za kiraia iinnaendelea kutumia mbinu bunifu ili kuchochea maendeleo ya watu. Tuna nia ya kuwa na mijadala inayozingatia watu. Kama sekta ya mashirika ya kiraia, tunaelewa kwamba tunaweza tu kutekeleza masuluhisho ya kimaendeleo kwa sauti za watu. Ushiriki wa watu katika maendeleo yao na kuwa na sauti juu ya changamoto zao ambazo ni muhimu zikapatiwa utatuzi. “ameongeza,

Katika hatua nyingine Kiwanga amezungumzia suala la mabadiliko ya tabia nchi ambapo amesema upo uwezekano wa kuwepo na uhaba wa chakula kutokana na uhaba wa uzalishaji wa mazoa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Norwegian Church Aid (NCA), Berte Marie Ulveseter amesema kuwa NCA kwa kushirikiana na LSF na Jukwaa la Kilimo lisilo la Kiserikali (ANSAF) watakuwa wenyeji wa kikao cha saa 3 katika wiki ya AZAKi iliyopewa jina la ‘KUKUZA MIKOPO YA 10% YA LGA KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU’

“Kikao chetu kinalenga kujadili athari za mikopo inayotolewa na Serikali katika maisha ya watu na maeneo yanayopendekezwa kuboreshwa. Pia Kikao hicho kitahusisha kutoa shuhuda kutoka kwa wajasiriamali waliofanikiwa’’, amesema.

Naye Mkuu wa kitengo cha Sekta ya Umma Benki ya Stanbic Doreen Dominic amesema kuwa kama Sekta Binafsi wanalojukumu kubwa la kuwanyanyua wananchi katika shuguli za kiuchumi kwa kuwawezesha katika kazi zao za uzalishajimali zikiwemo Biashara.

Amesema kwa sasa Benki hiyo inatambua kuwepo kwa juhudi kubwa zinazofanywa na wadau wa maendeleo na kwamba watahakikisha wanaunga mkono juhudi hizo ili kuendelea kuisaidia jamii ya watanzania.

“Tunatambua kuwa Kuna uwekezaji mkubwa nchini Sasa tunahitaji kuwanyanyua wananchini wakiwemo wafanyabiashara kwenda juu ili kuweza kupata fursa zinazotokea katika nchi yetu kwa Sasa”,amesema Doreen.
Share To:

Post A Comment: