Na Gift Mongi Moshi

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu  Ummy Nderiananga amewahimiza wadau wa maendeleo na watu binafsi kuendelea kushirikiana na serikali kwa kuchangia vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa.


Ummy amesema hayo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua ghala la kuhifadhi vifaa vya misaada ya kibinadamu wakati wa maafa Kanda ya Kaskazini  lililopo maeneo ya Chekereni, Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.


Amesema uungwaji mkono wa serikali kutoka kwa wadau unasadia wananchi kufikiwa na huduma kwa haraka kutokana na majanga yaliyojitokeza ambayo husabababisha madhara kama vifo, ulemavu wa kudumu, mali kuharibika pamoja na miundombinu.


“Nitoe wito kwa wadau na watu mbalimbali ambao wanaguswa kushirikiana na serikali kwa kutoa vifaa wafanye hivyo pengine ngazi ya Wilaya, Mkoa na hata kijiji ili tuwe navyo vya kutosha ili yanapotokea tunatoa msaada kwa haraka,” amehimiza Ummy.


Pia amesisitiza utunzwaji wa magahala hayo hatua itakayosaidia vifaa hivyo kudumu kwa muda mrefu na kuwa tayari kutumika pindi vinapohitajika katika maeneo yenye maafa.


"Naomba vitunzwe ili viweze kuwa na maana pindi vitakavyohitajika maa a visipotunzwa ni sawa na Kama hakuna vifaaa hivyo"alisisitiza Ummy


Aidha ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro kwa utayari wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa wananchi wanaokumbwa na maafa kwa lengo la kuwasaidia kurejea katika hali yao ya awali.


Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Kilimanjaro ambaye ni Afisa Mifugo katika Mkoa huo   James Shao amesema ghala la Kanda ya Kasikazini linahudumia Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga.


MWISHO

Share To:

Post A Comment: