Na,Jusline Marco;Arusha


Naibu kamishna wa kodi za ndani kutoka katika Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA,Swalehe Garugaba amesema kuwa wadau wa sekta ya utalii ni kundi muhimu katika masuala ya Kodi na wapo tayari kuwasikiliza ili kutambua changamoto za kibiashara zinazo wakabili katika suala la ulipaji kodi.

Garugaba ametoa kauli hiyo katika mkutano wa pamoja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na wadau wa Utalii, kujadili uelewa wa pamoja juu masuala ya kikodi na kusikiliza changamoto zinazoikabili sekta hiyo.

Amesema Mamalaka hiyo imeendelea kuweka mikakati na miundombinu ya ulipaji kodi kwa wateja wake ili kurahisisha ufanyaji wa biashara kwa wafanyabiashara wa Tanzania bara na visiwani ambapo amesema kukutana na wadau hao ni katika kuwafanya wafanyabiashara wa sekta ya utalii kufanya shughuli za utalii kwa uharahisi na kupunguza mlundikikano wa kodi.

"Sisi tunakusanya kodi lakini wadau muhimu wanao lipa Kodi moja wapo ni sekta ya utalii,na kwa kikao hiki tunaamini kitazaa matunda"Alisema

 "tupo katika muendelezo wa kukutana na makundi ya walipa kodi lengo likiwa ni kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo zikiwemo za kibiashara pamoja na kikodi,"alisema Byarugabe.


Naibu huyo amesema, kwa kufanya hivyo hali ya mapato nchini inazidi kuongezeka kwani hali hiyo ni matunda yatokanayo na ushirikiano baina ya TRA na wateja wake kutoka sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Kamishna wa bodi ya mapato Zanzibar,Yusuph Mwenda alisema
sekta ya utalii ndiyo inawezesha kukuza uchumi wa Zanzibar kwa zaidi ya asilimia arobaini kutokana na ushirikiano uliopo kurahisisha ukusanyaji wa kodi kwa wateja wake.

Mwenyekiti wa chama cha wakala wa utalii Tanzania (TATO)Henry Kimambo amesema kwa sasa changamoto za kimfumo ikiwemo kodi ya VAT ya Tanzania Bara ambayo ni asilimia 18 tofauti na Zanzibar ni asilimia 15 .

Ameongeza kuwa kutapitia mkutano huo utaweza kupitia baadhi ya sera ambazo zimekuwa changamoto katika shughuli zao za utalii hiyo na kuwaonyesha taswira kamili.

"Na leo tumekutana jijini Arusha kuwasikiliza changamoto za wadau wa sekta ya utalii ambapo tutapata fursa ya kuwaeleza njia nzuri ya kurahisisha kufanya shughuli zao za utalii nchini kote bila usumbufu kwa pamoja na wageni wanaofika nchini,"alisema.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: