Mwanahabari Frank Mbunda, enzi za uhai wake
 

Na Dotto Mwaibale 

Mwandishi wa Habari Mwandamizi, Frank Mbunda amefariki dunia leo Oktoba 16, 2022 Hospitali ya Mkoa General Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kufikishwa jana jioni.

Mtoto wa Marehemu Ashery Mbunda amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuwa taratibu za maziko zinafanyika Makole Dodoma nyumbani kwa mlezi wake wa Kiroho.

Mke wa marehemu, Yunice Mbunda amesema kesho Oktoba 17 itafanyika Misa ya kumuombea marehemu katika Kanisa la Anglikana Makole Dodoma na kesho kutwa Oktoba 18, 2022 mwili wake utasafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Dar es Salaa ambako taratibu za mazishi yake zitafanyika.

Marehemu Frank Mbunda ameacha mjane na watoto wanne, wakike wawili na wakiume wawili.

Frank Mbunda enzi za uhai wake amewahi kuandikia magazeti mbalimbali na hadi kifo chake alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kinarani Co.General Publishers and Priting iliyokuwa ikichapisha gazeti la Tanganyika Tanzania.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: