SASA ZIMEBAKIA TIKETI 22 NA vifurushi vya vifaa vya nyumbani 22 kutoka Hisense. 

Baadhi ya Washindi wa Safari ( iliyolipiwa kila kitu ) ya kwenda QATAR kushuhudia kombe la Dunia , Promosheni ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense ( Droo ya Nne ) katika picha ya pamoja muda mchache baada ya kukabidhiwa mfano wa Tiketi zao. 


Mwalimu Caren Jumbe Mkazi wa Buza Jijini DAR eS Salaam ( kulia ) akionyeshwa vifaa vya Hisense alivyojishindia ambavyo ni TV inchi 50 , Friji , Microwave na Subwoofer . Kushoto ni Meneja wa Wateja Maalum wa Tigo Pesa Bi. Mary Rutta


Hawa hapa baadhi ya washindi wa WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense Droo ya Nne 

Na Mwandishi Wetu.

Oktoba  28, 2022,  Kampuni inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya WAKISHUA TWENZETU QATAR na Hisense kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wametoa tiketi 28 za kwenda Qatar kushuhudia kombe la Dunia na washindi 8 wa zawadi ya Vyombo vya ndani kama vile Friji , Spika za Mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave .

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Ruta amesema kuwa

" Hawa washindi wa leo wamepatikana kwenye Droo yetu ya wiki ya nne ya promosheni yetu , walifanya miamala kama kulipa bili , kufanya malipo ya kiserikali , kupokea pesa kutoka nchi za nje , benki , mitandao mingine , LIPA KWA SIMU , kununua muda wa maongezi , kuchukuabmikopo ya TigobPesa na huduma nyingine mbalimbali za Tigo Pesa ambapo baada ya kufanya ivyo waliingia kwenye droo na mwisho wa siku kuibuka washindi wa Kampeni hii Ya WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE , Tunawasihi wateja wetu endeleeni kufanya miamala na Tigo Pesa ili kuibuka mshindi , na leo tumepata idadi ya washindi 28 wanaoenda kushuhudia kombe la dunia mubashara na washindi washindi 8 wanaojipatia kifurushi cha vifaa vya ndani vya Hisense.

 " Tumebaki na tiketi 22 za kwenda QATAR kushuhudia kombe la dunia , na bidhaa 22 za vifaa vya ndani kutoka Hisense , kwahyo nawasihi mfanye miamala mingi na kutumia huduma za Tigo Pesa ili kuibuka mshindi wa zawadi hizi zilizobaki " Alimalizia.

Naye kwa upande wake Afisa Masoko wa Kampuni ya HISENSE Bwn. Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense inatoa ofa ya punguzo la 20% katika maduka yao yote kwa mteja atakayenunua bidhaaa na Kulipia kwa Tigo Pesa " Alimalizia 

Naye mmoja wa Washindi wa Vifaa vya ndani ambavyo ni Tv inchi 50 , Friji , Microwave na Subwoofer kutoka chapa ya Hisense  Bi. Caren Jumbe Mkazi w a Buza akielezea furaha yake baada ya kukabidhiwa Zawadi zake amesema kuwa 

" Kwakweli sikuamini kabisa , maana nlipigiwa simu na namba 100 ya Tigo na kuambiwa kwamba nimeshinda promosheni , nilifikiri ni matapeli lakini baadae nkaelekezwa kwamba ijumaa nifike hapa makao makuu kuchukua zawadi zangu na nimefika nimeziona zawadi zangu kwakweli sijui nisemeje lakini nawasihi watanzania msipuuze hii kampeni ya wakishua ni kweli kabisa , Fanyeni miamala kwa wingi maana zawadi bado zipo na sio vifaa vya ndani tu huenda labda naww ukaibuka mshindi wa safari ya kwenda Qatar kushuhudia mechi za kombe la dunia ukiwa umelipiwa kila kitu na Tigo "  Alimalizia . 

Naye mmoja wa washindi wa Safari ya kwenda Qatar Bwn. Kassim Abeid amesema kuwa anafuraha sana kuwa mshindi na furaha yake kubwa ni kwenda kuwaona LIVE  wachezaji wake pendwa wakicheza mpira .

" Hakika hii ni furaha iliyoje , asante sana Tigo na Hisense mmefanya makubwa nawasihi Watanzania wafanye miamala kwa wingi huenda nao wakaibuka washindi kama ilivyotokeza kwangu maana sikutaraji " Alimalizia Bwn. Kassim 


Share To:

Adery Masta

Post A Comment: