1.Ugonjwa wa Ebola ni nini?

Ugonjwa utokanao na kirusi cha Ebola ni ugonjwa hatari wenye uwezo wa kusababisha kifo kwa asilimia 90.  Shirika la afya duniani, WHO katika tovutiyake inasema kwa mara ya kwanza ulibainika mwaka 1976 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan. Chanzo cha kirusi hiki hadi sasa hakijulikani lakini popo aina ya (Pteropodidae) wanaonekana kuwa wabebaji wa kirusi hicho,kwa mujibu wa ushahidi uliopo sasa.

 2. Binadamu anaambukizwa vipi kirusi cha Ebola?

Mlipuko wa sasa huko Afrika Magharibi kwa kiasi kikubwa umesababishwa na maambukizi ya binadamu kwa binadamu. Maambukizi hutokea pindi mtu anapoambukizwa kupitia sehemu wazi ya mwili wake majimaji ya mgonjwa wa Ebola. Mathalani matapishi, choo, mate, mbegu za kiume, au Semen na damu. Maambukizi yanaweza kutokea pia iwapo ngozi yenye uwazi ya mtu asiye na ugonjwa huo itakumbwa na maji maji yenye kirusi yaliyomo kwenye nguo chafu za mgonjwa, mashuka au sindano zilizotumika.

Zaidi ya wahudumu 100 wa afya wamekumbana na mazingira yenye majimaji kutoka mwili wa mgonjwa wa Ebola pindi wanapokuwa wanatoa huduma kwa wagonjwa hao. Hii hutokea iwapo hawana mavazi stahili ya kujikinga au hawakuzingatia taratibu za kujikinga pindi wanapohudumia wagonjwa. WHO inataka watoa huduma afya katika ngazi zote iwe hospitali, kliniki,zahanati au vituo vya afya wapatiwe taarifa juu ya ugonjwa wa Ebola, unavyoambukizwa na wazingatia mbinu za kuzuia kuenea kwake.

WHO haishauri familia au jamii kuhudumia wagonjwa wanaoweza kuwa na dalili za Ebola majumbani mwao. Badala yake wanataka wapate huduma hospitali au kituo cha afya. WHO imesema maambukizi mengine yameripotiwa kwenye mazishi au mila za mazishi. Katika shughuli hizo waombolezaji wanagusana na mwili wa marehemu na hivyo kujiweka hatarini. WHO inasihi mazishi ya waliofariki dunia kwa Ebola yafanyike kwa kiwango kikubwa cha kujikinga kwa kuvaa mavazi maalum na wanaofariki dunia wazikwe mara moja. Mazishi hayo yafanyike chini ya usimamizi wa wataalamu wa afya.

Mtu anaweza kuambukiza kirusi cha Ebola iwapo damu yake au majimaji ya mwilini yana kirushi hicho. Hivyo basi, wagonjwa wa Ebola wanapaswa kuwa chini ya uangalizi wa hali ya juu kutoka kwa wataalamku na wafanyiwe uchunguzi kuhakikisha kirusi hakipo tena mwilini kabla ya kurejea nyumbani.

Mtaalamu wa afya baada ya kipimo anabaini kuwa mgonjwa ni salama kurejea nyumbani kwa kuwa amepona na hana tena kirusi, hawezi kuambukiza wengine.Hata hivyo wanaume ambao wamepona ugonjwa huo bado wanaweza kuambukiza kupitia njia ya kujamiiana ndani ya wiki saba baada ya kupono. Hivyo wanashauriwa kutoshiriki tendo hilo ndani ya wiki saba baada ya kupona. Na iwapo atalazimika basi ni lazima atumie mpira wa kiume.

3. Nani yuko hatarini zaidi?

Wakati wa mlipuko, walio hatarini zaidi kuambukizwa ugonjwa wa Ebola ni:

  • Wahudumu wa afya;
  • Wanafamilia au watu wengine walio karibu na mgonjwa wa Ebola
  • Waombolezaji ambao wanashika maiti ya mgonjwa wa Ebola kama sehemu ya ibada ya mazishi.

 4. Dalili za Ebola ni zipi?

Homa ya ghafla, uchovu wa kina, maumivu ya misuli, maumivu ya kichwa, koo kukauka. Hii hufuatiwa na kutapika, kuhara, vipele, figo kushindwa kufanya kazi, halikadhalika ini, na wakati mwingine damu kuanza kuvunja ndani na nje ya mwili.

Baada ya dalili hizo kuonekana, ugonjwa unaweza kubainika kati ya siku Mbili hadi 21 na hapo ndipo mgonjw anaweza kuambukiza wengine. Wakati ugonjwa haujabainika, mtu hawezi kuambukiza mtu mwingine. Thibitisho la ugonjwa huu hupatikana maabara pekee.

5. Je kuna tiba au chanjo?

Kwa sasa hakuna dawa au chanjo iliyosajiliwa kutibu ugonjwa wa kirusi cha Ebola. Hata hivyo dawa kadhaa zinaendelezwa na WHO imeridhia tiba ya majaribio kutumika kutibu wagonjwa.Share To:

Post A Comment: