Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi PURA na Wajumbe wa Kamati za Bodi Wakiwa Katika Picha ya Pamoja Mara Baada ya Kumaliza Ziara katika Mitambo ya Kuchakata Gesi Asilia iliyopo Madimba.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PURA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia iliyopo eneo la Madimba - Mtwara tarehe 08 Oktoba, 2022. Kutoka kushoto ni Bw. Yona Killagane (Mjumbe), Bi. Beng'i Issa(Makamu Mwenyekiti wa Bodi), Bw. Halfan R. Halfan (Mwenyekiti wa Bodi), Mha. Charles Sangweni (Katibu wa Bodi), Prof. Josephat Lotto (Mjumbe), na Mha. Ramadhani Masudi (Mjumbe).


Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi PURA wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mtaalamu kutoka kampuni ya Maurel and Prom, Bw. Hussein Chitemo.


Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi PURA, Wajumbe wa Kamati za Bodi, Menejimenti na Baadhi ya Maafisa wa PURA na GASCO katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ziara katika Mitambo ya Kuchakata Gesi Asilia iliyopo Madimba



***********************

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) ipo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwa lengo la kuogeza uelewa wa shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka hiyo.

 Bodi hiyo imeanza ziara leo tarehe 08 Oktoba, 2022 kwa kutembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia na visima vya kuzalisha gesi asilia vilivyopo eneo la Mnazi Bay chini ya uendeshaji wa kampuni ya Maurel & Prom Exploration Production Tanzania Ltd. 

Bodi pia imetembelea mitambo ya kuchakata gesi asilia iliyopo eneo la Madimba inayoendeshwa na GASCO ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Kituo cha Kupokea Gesi Asilia kwa ajili ya kufua umeme kilichopo Mtwara Mjini kinachoendeshwa na kampuni ya Maurel & Prom. 

Bodi hiyo yenye wajumbe watano imeambatana na wajumbe wa Kamati za Bodi, menejimenti ya PURA na baadhi ya wataalamu kutoka PURA.

 Akitoa neno katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya PURA, Bw. Halfani R. Halfani amesema kuwa ziara hiyo imekukuwa na manufaa makubwa hususan kwa wajumbe wapya wa kamati za Bodi walioteuliwa hivi karibuni ambao hawakuwa wamewahi kufika maeneo hayo.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: