Waziri  wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ameagiza vifa muhimu vya kupima ubora wa Maji kwenye maabara ya Maji Kanda ya Mtwara kuletwa mara moja.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Aweso alisema uwekezaji uliofanywa na serikali kwenye ujenzi wa miundombinu uendane na ukubwa wa kazi zinazofanyika katika upimaji wa ubora wa maji.

Aweso ametoa maagizo hayo alipotembelea jengo la Maabara ya Maji kanda ya Mtwara na kugundua kuna baadhi ya vifaa vya vipimo muhimu ambavyo hulazimika kufanyika Dar Es Salaam badala ya kumaliza kazi zote za upimaji hapohapo kanda ya Mtwara.

Share To:

Post A Comment: