Na Fredy Mgunda, Iringa.


JUMLA ya watumishi 53 wapya katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga wameahidi kufanya kazi kwa kujituma,kuwawabunifu na kufuata taratibu zote walizopewa na viongozi ili kuhakikisha Halmashauri hiyo inafanya vizuri kwenye idara zote walizopangiwa.


wakizungumza mara baada ya kupewa maelezo na sheria za utumishi wa UMMA walisema kuwa wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira kwa vijana katika sekta mbalimbali.


Walisema kuwa watafanya kazi katika Halmashauri hiyo kwa ubunifu mkubwa ili kuomuonyesha Rais na watanzania kwa ujumla kuwa wanaitenda haki nafasi waliopata kuajiliwa serikalini.


Walimalizia kwa kumshukuru mkurugenzi wa Mji wa Mafinga Happiness Laizer kwa kuwapokea na kuwapa ushirikiano huku wakimuahidi kufanya kazi kwa nidhamu kubwa na watakuwa wabunifu wawapo kazini.



Kwa uapande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Happiness Laizer alisema kuwa kupatikana kwa ajira hizo mpya katika Halmashauri hiyo kutapunguza baadhi ya changamoto zilizokuwa zinawakabili kwenye baadhi ya sekta ikiwemo elimu na afya.


Laizer alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira 53 wa mwezi wa sita na wa saba.


Alisema kuwa watumishi 22 wanaenda kwenye sekta ya afya,walimu wa shule ya msingi watatu, walimu wa sekondari 11,Watendaji wa mitaa kumi 10, madereva wanne na masektari watatu.


Naye Afisa Utumishi na Utawala katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga Fredrick Kayombo alisema kuwa watumishi hao wapya tayari wamepewa maelekezo elekezi kuhusu sheria,kanuni na maadili ya utumishi wa umma.


Kayombo alisema kuwa lengo la kuwapatia muongozo watumishi wapya ni kuhakikisha wanaenda kufanya kazi vile ambavyo inapaswa kufanya kwa maendeleo ya wananchi wa Halmashauri ya mji wa Mafinga.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: