Godluck Mollel, Mwenyekiti UVCCM wilaya ya Kiteto aliyemaliza muda wake baada ya kuongoza kwa miaka mitano.

Hamza Mngia Mwenyekiti mpya wa UVCCM wilaya ya Kiteto aliyechaguliwa septemba 23,2022, na ataongoza kwa miaka mitano.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga akizungumza na wajumbe wa UVCCM Septemba 23,2022 kwenye uchaguzi uliofanyika Mjini Kibaya.

Wanachama wa UVCM wilaya ya Kiteto wakaifuatilia jambo kwenye uchaguzi wa jumuiya hiyo uliofanyika Septemba 23,2022 mjini Kibaya.

John Walter -Kiteto. 


Wananchi wilayani Kiteto mkoani Manyara, wameomba kikosi cha kuzuia na Kupambana na Rushwa RAKUKURU, kuingilia kati chaguzi za viongozi zinazoendelea wakisema, viongozi wanaotokana na Rushwa muda mwingi wanapambana kurejesha fedha walizotumia kuingia madarakani kuliko kuwatumikia wananchi.

Wamesema kiongozi anayeingia madarakani kwa rushwa wakati wote anapambana kurejesha fedha zake alizotumia na kuwasahau wapiga kura wao hivyo ili kunusuru hali hiyo TAKUKURU waingilie kati chaguzi zote zenye maslahi na wananchi.

Akizungumza hayo Neema Urasa mmoja wa wananchi wilayani Kiteto amesema kwa muda mrefu sasa huduma za jamii zimekuwa zikisuasua kutokana na upatikanaji wa viongozi wa aina hiyo.

"Leo hii ukiangalia hakuna huduma ya jamii ambayo wananchi hatulalamiki...na hii yote inachangiwa na kuwa na viongozi ambao wanajali maslahi yao binafsi badala ya kumwangalia aliyemweka madarakani" alisema Urasa.

Akizungumzia Rushwa katika Uchaguzi, Damas Emmanul alisema wananchi wanashindwa kuwapata viongozi wao wa kuwasaidia  kwa kudanganywa na Rushwa na kujikuta wakichagua wasio na mwito wavkuwatumikia.

Kwa upande wake Naftari Stephano alisema Rushwa ni adui wa uchaguzi kwani mara zote kiongozi anayepatikana hapo hatokani na matakwa ya wananchi bali anachaguliwa kwa kutumia fedha ambazo akiingia madarakani huishia kutumia muda meingi kuzirejesha kuliko kuwatumikia wananchi.

"Hapa unawezaje kumdai kiongozi huduma wakati alikupa pesa...wananchi pamoja na shida zetu tunalazimika kuwa kimpa mpaka wakati mwingine wa uchaguzi" alisema Stephano Mwananchi wa Kibaya.

Mkuu wa Kuzuia na kupambana na Rushwa Kiteto, Venance Sangawe akizungumzia rushwa kwenye uchaguzi wa UV-CCM alionya wajumbe hao kuacha kujihusisha na Rushwa akidai inawapa upofu wananchi katika maamuzi.

"Msikubali kutoa Rushwa ninyi mliopata fursa ya kuchagua viongozi...Rushwa inafanya mtu aifanye maamuzi sahihi na mtateseka sana kwa miaka mitano, hata kama umechukua kumbuka haya maneno kuwa nimewakataza chagueni kwa kutumia akili zenu ili mpate viongozi makini" alisema Sangawe.

Katibu wa CCM Kiteto, Denis Mwita, alisema CCM Kiteto wameanza uchaguzi wa Jumuia zake leo Septemba 23.2022 kwa siku tatu mfululizo kuwapa wajumbe hali ya kuchagua viongozi wenye maslahi na wananchi akidai kuwa nafasi hiyo ni muhimu kwa sasa.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga akizungumza na wajumbe hao aliwataka kuwa pamoja na nafasi walizonazo wajiimarishe kiuchumi kwa kufanyakazi za kilimo ambacho kwa sasa kina tija.

"Nimekuja na mikakati pamoja na nafasi hizi mlizonazo vijana tulime, ile kazi mnayopenda ya bodaboda Kiteto msitegemee kupata mikopo hiyo tutawakopesha mkalime tena kilimo chenye tija"

Mwenyekiti wa UV-CCM anayemaliza muda wake amesema amepambana na Rushwa katika kipindi chake na kukiri kuwa inachangia kuifisha maendeleo ya wananchi

Aliwataka watakaoingia madarakani kuhakikishe wanakabiliana na Rushwa kwani mpaka sasa bado inawafumba macho wanachama kutowapa haki wenye sifa na badala yake wanachagua kwankurubuniwa kwa fedha.
Share To:

Post A Comment: