Na Ahmed Mahmoud ; Arusha

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha wamehoji Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ipo wapi baada ya Uchaguzi ndani ya Chama hicho Ngazi ya Jumuiya kugubikwa na Rushwa wazi wazi hadi vyooni.

Akizungumza mmoja wa wanachama wa chama hicho aliyekataa kutajwa jina hadharani amesema Taasisi hiyo imekuwa kimya bila kufuatilia matukio yanayoendelea ndani ya chaguzi za chama kutokea ngazi ya matawi kata hadi Wilaya ambapo kumekuwepo utoaji wa rushwa za waziwazi jambo ambalo sio mustakabali mzuri wa chama hicho.

Amesema zoezi la wagombea wenye majina makubwa wamekuwa wakitumia watu kugawa fedha na majiko ya magesi kwa wanachama ili kupanga safu za uongozi ndani ya chama hicho jambo ambalo siku za usoni litakuja kukigharimu chama hicho na kuhoji Taasisi hiyo imeshindwa kufuatilia masuala mazima ya rushwa ndani ya chama hicho.

Mwanachama huyo ameendelea kuwashukuru wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi  kwa kuonyesha ukomavu na kuikataa rushwa iliyokuwa ikitolewa ndani na nje ya ukumbi wa uchaguzi hadi ndanni ya vyoo wazi wazi hadi msimamizi wa uchaguzi huo Anna Msuya baada ya uchaguzi wakati akishukuru na kufunga uchaguzi huo kutamka waziwazi kuwa kulikuwa na vitendo vya rushwa hadikuwatoa nje ya ukumbi wajumbe wawili Bi. Asia Mkali na Bwana John Mchasu waliokuwa wanagawa rushwa ndani ya ukumbi hadi meza kuu.

Akiongea Mara Baada ya Uchaguzi huo Msimamizi wa uchaguzi huo Anna Msuya amesema uchaguzi huo umeonyesha mustakabali mwema na kuonyesha nguvu ya wanachama kukataa vitendo vya rushwa na kuonyesha ukomavu kutopangiwa wa kufuata maelekezo. 

Akitangaza matokea hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mjumbe wa Halmashauri kuu Anna Msuya Ally Mwinyimvua  amepata kura 212  huku Meya Mstaafu Gaudence Lyimo akiambulia 61 na Bertha Laizer kura 1 hivyo kumtangaza Ally Mwinyimvua kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi kwa kipindi cha pili.

Hatahivyo Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha James Ruge alipotafuta kwa njia ya simu alijibu kuwa hakuna tukio hilo kwani wanapopewa Taarifa huzifanyiakazi na kutaka mwandishi kutoa taarifa kabla ya kuuliza au kuhoji suala lolote kwa TAKUKURU mkoa.

"Nauliza ulileta taarifa kwetu hata uhoji tukio hilo kwetu suala la rushwa ni jukumu la wananchi wote hivyo kama ulitupa taarifa tueleze kwanza ndipo tujipo sasa hakuna tukio hilo akijibu kwa kufoka"



Share To:

Post A Comment: