Na,Tata Jacob;Mara

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wilaya Tarime Mkoani Mara imeanza kusikiliza Shauri upande wa utetezi dhidi ya mshtakiwa wa kesi ya jinai Namba CC 26 ya mwaka 2022 inayomkabali mwenyekiti wa kijiji cha Nyabichune Mgaya Kisire kwa kosa la kumjeruhi mwananchi wake Bhoke Peter ikiwa ni pamoja na kuendesha opareshini ya kufukia shimo analochimba madini mama huyo na kubomoa Choo chake Nyumbani kwake ambapo mshtakiwa amekana kutenda kosa la kumjeruhi mama huyo.

Kesi ya jinai namba CC 26 ya mwaka 2022 imeanza kusikilizwa kwa upande wa utetezi ambapo hii leo shahidi wa kwanza wa kesi hiyo ambaye ni mshtakiwa Magaya kisire amejitetea mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakamama ya wilaya Tarime Mhe. VERONICA SELEMANI ambapo amekana kutenda kosa la kumjeruhi mama Bhoke Peter ambaye ni mlalamikaji huku akisema kuwa alikuwa akitekeleza majukumu yake ya kikazi kama kiongozi wa eneo hilo hivyo hakumjeruhi ndugu mlalamikaji Bhoke Peter kwa namna yoyote ile.

Aidha mshtakiwa Mgaya kisire ameiambia mahakama kuwa shughuli hiyo ya ufunikaji wa mashimo ilikuwa inasimamiwa na vyombo mbalimbali ikiwemo Jeshi la polisi waliokuwa wakililinda usalama wakati shughuli hiyo ikiendelea hivyo kama angetenda kosa la kumjeruhi mama huyo basi maafisa wa polisi wasingemuacha ama kumruhusu kuondoka eneo hilo bali wangemshikilia kwa kutenda kosa hilo mbele yao kama walinzi wa amani .

Katika hatua nyingine pia shahidi huyo wa kwanza upande wa utetezi Mgaya Kisire ambaye ndiye mshtakiwa wa kesi hiyo ameiomba Mahakama itende haki na imuachie huru kwa kuwa hakutenda kosa hilo

Mahakama imeahairisha shauri hilo hadi Tarehe 10 mwezi October mara baada ya kusikiliza maelezo ya shahidi wa kwanza wa kesi hiyo ambapo Hakimu mkazi mwandamizi veronica selemani amesema siku hiyo Mahakama itaendelea kusikiliza mashahidi wengine waliobaki kwa upande wa mshtakiwa.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: