Na Fredy Mgunda, Iringa.



Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amesema Mwenge wa Uhuru umezindua miaradi ya bilioni moja na Milioni mia tisa(1,600,000,000) katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.


Akizungumza mara baada ya miradi yote kuzinduliwa mkuu wa wilaya ya Iringa Moyo alisema kuwa miradi ambayo imezinduliwa ni madarasa mawili ya shule ya sekondari Tangamenda ya mradi wa 5441TC RP, Isakalilo sekondari kwa kuweka jiwe la msingi,kuweka jiwe la msingi hospital ya Frelimo, kuzindua barabara ya mtwivila darajani Ikonongo kwa kiwango cha lami kilometa 1.4 na miradi ya huduma ya jamii na kiichumi kwa maendeleo ya wananchi wa kikundi cha Ebenezer.


Moyo alisema kuwa kuwa anawashukuru wakimbiza mwenge wa Uhuru kwa kuikubali miradi yote kwa ubora ambao unatakiwa kutekelezwa kulingana na thamani ya fedha.



Alisema kuwa anawapongeza wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kujitokeza kwa wingi kuulaki mwenge wa Uhuru ulipokuwa unakimbizwa kwenye Halmashauri hiyo.


Lakini pia mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na viongozi wakimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa kwa ajili ya kuimarisha ubora ya miradi na utumishi wa UMMA.


Kwa upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa,Sahili Nyanzabara Geraruma alisema kuwa viongozi Manispaa ya Iringa wamejitahidi kusimamia miradi ambayo inatekelezwa kwa fedha za serikali kuu na serikali za mitaa kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi.


Geraruma alisema kuwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mkuu wa wilaya ya Iringa wanatakiwa kuwa makini kuangalia namna ambavyo miradi yote inayotekelezwa ili kukidhi vigezo kulingana na thamani ya fedha ilayotolewa na serikali.

Share To:

Post A Comment: