Mufti  wa Tanzania Sheikh Dk. Abubakar Zubeir Ally Mbwana (katikati) akizungumza wakati akiongoza maelfu ya Waislam mkoani Singida katika hafla ya kuzindua Mfuko wa Maendeleo wa Mufti katikahafla iliyofanyika leo Septemba 19, 2022 Stendi ya zamani mjini haaapa. Kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Nuhu Jabir Mruma na kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issah Nassoro Issah.
Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issah Nassoro Issah. akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mbunge wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi wa mfuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mfuko huo.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo wa Mufti akizungumzia umuhimu wa mfuko huo na jinsi utakavyokuwa ukifanya kazi.

Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Bakwata Taifa, Sheikh Ally Hamisi Ngorike akizungumza.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Bakwata Taifa, Sheikh Hamis Mataka akizungumza.
Dua ikifanyika.
Bi. Salha Amir mkazi wa Iramba, akimkabidhi Mufti Zubeir taarifa ya Hospitali yake aliyoikabidhi kwa Mfuko huo wa Maendeleo wa Mufti.
Mufti Zubeir akionesha taarifa hiyo.

 Mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kutoka Kata ya Ihanja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Bakwata Mkoa wa Singida, Ahmed Misanga akimkabidhi Mufti Zubeir Sh. 300,000 kwa ajili ya kuchangia mfuko huo.
Sehemu ya Taswira ya uzinduzi huo.
Mufti Zubeir akiagana na viongozi mbalimbali baada ya kuzindua mfuko huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Bingwa wa kusoma Quran Ibrahim Mtigo akisoma Quran katika uzinduzi huo.
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhajj Burhan Mlau akizungumza wakati akiwatambulisha wageni mbalimbali kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali na Masheikh wakiwa  jukwaa kuu wakati wa uzinduzi wa mfuko huo.
Mwenyekiti wa Bakwata Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii akipeana mkono na Mufti Zubeir baada ya kutoa nyumba yake ya vyumba saba na eneo la ardhi kwa ajili ya mfuko huo.

Dotto Mwaibale na Philemon Mazala, Singida

MUFTI wa Tanzania Sheikh Dk. Abubakar Zubeir Ally Mbwana ameongoza maelfu ya waislam mkoani Singida katika hafla ya kuzindua Mfuko wa Maendeleo wa Mufti ambao ni muhimu kwa maendeleo ya waislam nchini.

Akizindua mfuko huo leo Septemba 19, 2022 katika hafla iliyofanyika Stendi ya Mabasi ya Zamani mjini hapa Mufti Zubeir aliwataka waislam kote nchini kujenga tabia ya kujitolea na kutoa kwa kile walichonacho kwa ajili ya kuendeleza dini ya kiislam.

Alisema Mtume Muhammad (SAW ) alipokuwa akiutangaza uislam na kuukumbatia kila aliyekuwa nacho alitoa halikadharika na waliokwenda hija walifanya hivyo mpaka uislam ukafika ulipofikia.

"Watu walitoa mali zao mbalimbali kwa ajili ya kuipigania dini ya kiislam hivyo na sisi tusiwe nyuma kufanya hivyo" alisema Mufti Zubeir.

Alisema jambo hilo la kuchangia mfuko huo si la ujanja ujanja bali lina mpango kamili hivyo watumie fursa hiyo kwa ajili ya kutoa kwa maendeleo ya waislam na dhawabu zao watazikuta mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mufti Zubeir aliwahimiza waislam kufanya hivyo kwani Mungu ataona, waislam wataona na Mtume Mohamad ( SAW)ataona na akaeleza kuwa waislam hawatakiwi kuwa na tabia ya kuombaomba na kuwa ni heri ya kuwa na mkono wa kutoa kuliko wa kupokea kwani waislam wa Tanzania ni matajiri ambao kilammoja hashindwi kutoa Sh.10,000 kwa mwezi kama alivyo jitolea mwanamke Hadija anaye simuliwa katika kitabu kitakatifu cha quran.

Mufti Zubeir aliwataka waislam kuondoa dhana ya kuwa michango inayotolewa haiendi kufanya maendeleo badala yake wawe na imani  akitolea mfano baadhi ya wenzao ambao hakuwataja kuwa  wamekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kutokuwa na mtazamo huo.

"Wenzetu wakizungumza jambo wanakusanya pesa na wakiamua linakuwa, mimi nina ushahidi ipo siku nitawaambia lakini sisi tukizungumza jambo na Imam msikitini, baadhi ya viongozi kwenye kata, wilaya na mkoa wanalipinga" alisema Mufti.

Alisema kumekuwa na changamoto  ya watu  waliostaafu au kuondolewa kazini kwenda misikitini na kujifanya wanajua kila kitu "wataaalam' huku wakizungumza kiingereza na kuwavuruga waislam ambapo alieleza kuwa jambo hilo sio zuri.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilayaya Singida, Mhandisi Paskas Mulagiri alisema Serikali imekuwa ikiamini kwa sehemu kubwa sana kuwa amani na utulivu uliopo hapa nchini ni kwa sababu ya kazi kubwa inayofanywa na viongozi wa dini kwa kuliombea taifa na maadili ya kidini ambayo yanajenga amani na upendo.

Muragili alitumia nafasi hiyokuwashukuru viongoziwa dini kwa kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha waumini wao kwenye zoezi la kitaifaa la Sensa ya Watu na Makazi ambalo lilipata    mafanikio makubwa na Mkoa wa Singida ulipata zaidi ya asilimia 100.

Aidha Muragili alimpongeza Mufti wa Tanzania Sheikh. Dk.Abubakar Zubeir kwa kuwa na maono ya kuanzisha Mfuko wa Maendeleo wa Mufti (MDF) ambao ni mkombozi mkubwa kwa Serikali kwani unakwenda kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Katika uzinduzi wa mfuko huo viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam, Serikali, wafanyabiashara, watumishi wa umma, watu binafsi, wananchi na wanasiasa walijitokeza kuchangia mfuko huo miongoni mwao akiwa ni Bi. Salha Amir mkazi wa Iramba ambaye ameitoa Hospitali yake yenye vyumba zaidi ya 25 na ardhi yenye ekari 12.5 vyote vikiwa na thamani ya Sh.Bilioni 1 kwa ajili ya mradi wa mfuko wa maendeleo wa Mufti.

Wengine waliochangia mfuko huo ni Mwenyekiti wa Bakwata Mkoa wa Singida, Jumanne Nkii ambaye naye alitoa nyumba ya vyumba saba na eneo la ardhi na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambaye ametoa ahadi ya kutoa Sh.10 milioni akishirikiana na rafiki zake wadau wa maendeleo pamoja na Ahmed Misanga ambaye ni Mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida kutoka Kata ya Ihanja na Mjumbe wa Halmashauri Bakwata Mkoa wa Singida ambaye alitoa Sh.300,000.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: