Na,Andrew Chale; Kalambo.


Mkuu wa Wilaya ya Kalambo iliyoko Mkoani Rukwa, Mhe. Tano Mwera amewataka kuhakikisha Wazazi wanawapeleka watoto wao wote walio chini ya miaka Mitano kupata chanjo ya matone ya  Polio katika zoezi la siku nne, lililoanza rasmi Leo Septemba Mosi,2022.


Mhe. Tano Mwera ametoa kauli hiyo mapema leo wakati wa kuzindua zoezi hilo la chanjo ya Polio katika Kijiji cha Kisungamire,Wilayani hapa ambapo amesema ndani ya siku nne wawe wamehakikisha watoto wote walio chini ya miaka mitano wanapata chanjo.


"Ndugu zangu wa Kisungamire na Kalambo, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Samia Suluhu Hassan anatupenda sana na ndiyo maana anataka kuhakikisha afya za watanzania wote wakiwemo wanakisungamire pamoja wanakalambo wote zinaimarika, ndiyo maana zimeletwa hizi chanjo".

"tuhakikishe tunapata hizi chanjo bila kuchelewa, tuna siku nne tu hizi chanjo ziwe zimetembea kuhakikisha watoto wanapata chanjo hii."


Aidha, mbali ya kuzindua na kuhamasisha zoezi hilo la chanjo hiyo, Mhe.Tano Mwera amehamasisha zoezi la Sensa ambapo wale ambao  bado kuhakikisha wanafikiwa kama ilivyotangazwa na Serikali ikiwemo kupiga simu maalum katika zoezi linaendelea ikawemo la Watu na Makazi.



Mwisho.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: