Na Ahmed Mahmoud 


Wakati zoezi la sensa ya watu na makazi likitarajiwa kuanza kesho uhamasishaji kwa namna mbalimbali umeendelea kufanyika jijini Arusha ikiwemo nyimbo na ngoma za kitamaduni.


Uhamasishaji huo umefanyika wakati wa kukabidhi vikombe vya ushindi wa mashindano ya michezo kwa wanafunzi wa shule ya msingi (umitashumta) na shule za sekondari (umiseta) kwa mkuu wa mkoa wa Arusha.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vikombe vinne vya ushindi wa mpira wa kikapu, wa mikono na riadha mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela alisisitiza kujipanga kabla ya mashindano hayo.


“Tuhakikishe tunajipanga ipasavyo na kuzigawa shule kijiografia mfano Karatu kule tuandae vijana wa kesho kwenye riadha ili kuzisaidia timu zetu za Taifa kwa siku za usoni.


Nae Katibu Tawala mkoa wa Arusha Missaile Mussa amesema kwamba vijana hao wanahitaji kupewa moyo ili waweze kuitangaza mkoa siku za usoni kwani nafasi walioshika kitaifa 5 imeutangaza mkoa hivyo tujipanga kutoka hapo tulipo twende mbele zaidi


Awali akiongea katika hafla hiyo Afisa Elimu Mkoa Abel Mtupwa amesema pamoja na ushindi huo wamechukuwa maelekezo yote na kwenda kuyafanyiakazi ipasavyo na kuahidi mwakani kurudi katika nafasi tatu za juu sanjari na kukuza vipaji.


Amesema kwamba umoja na mshikamano wao utasaidia kuibua vipaji sanjsri na kuanzisha shule maalum kwa kila wilaya ili kuweza kuleta ushindani kwa timu zilizoshika nafasi za juu


Kwa upande wa wanafunzi waliotoka kwenye mashindano hayo yaliyofanyika Tabora, walieleza jinsi mashindano yalivyokuwa na namna yalivyotumika kuhamasisha sensa inayotarajiwa kufanyika kesho.

Share To:

Post A Comment: