Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Itagata baada ya kukagua  Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Itagata wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni mkoani hapa aliyoifanya jana.
Ukaguzi wa Skimu hiyo ukiendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiangalia Skimu hiyo wakati wa ukaguzi.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda ambaye ana kaimu nafasi ya ukuu wa wilaya ya Manyoni akizungumza katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Itagata.

Kaimu Mhandisi wa Umwagiliaji Mkoa wa Singida, Ponda Shabani akichangia jambo wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Umwagiliaji Kijiji cha Itagata, Stephano Mbonde, akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba wakati wa ukaguzi wa Skimu hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, 
Muonekano wa Bwawa la Skimu ya Itagata.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akiongoza viongozi mbalimbali  wakati wa ukaguzi wa Skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Itagata wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Itigi wilayani Manyoni.
Mkulima katika Skimu hiyo,  Amani Luaga akiwajibika katika shamba lake la vitunguu.
Mkulima katika Skimu hiyo, Omari  Shabaniakiwajibika.
Suzana William (kulia) na Masele Sona wakivuna vitunguu katika Skimu hiyo.
Muonekano wa Mahindi yaliyolimwa kwenye Skimu hiyo.
Waandishi wa habari wakiwajibika wakati wa ziara hiyo ya mkuu wa mkoa.
Mkulima katika Skimu hiyo Chacha Marwa (kushoto) na George Kampanda wakiruhusu maji kupita katika Skimu hiyo.
Ukaguzi wa Skimu hiyo ukiendelea.
Ukaguzi wa Skimu hiyo ukiendelea.
Muonekano wa Skimu hiyo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Itagata, Mwajuma Abrahaman akizungumza kabla ya kuanza kwa  mkutano huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Itagata,  Juma Jabiri, akifungua mkutano huo wa mkuu wa mkoa.

Mzee Said Mussa Ntanduwa Kijiji cha Itagata, akitoa kero yake mbele ya Mkuu wa Mkoa.
Mkazi wa Itagata,  Mussa Shabani akielezea changamoto yake ya kuporwa ng'ombe.
Wanananchi wa Itagata wakiwa kwenye mkutano huo wa mkuu wa mkoa.
Mkutano ukiendelea. 


 

Na Dotto Mwaibale, Itigi.

 

SERIKALI mkoani Singida imesema itawanyang'anya na kuyagawa kwa wengine wakulima waliopewa mashamba katika Skimu ya Umwagiliaji Itagata iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ambapo wametelekeza ekari 169 bila kuzilima.

Msimamo huo ulitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba baadaya kuitembelea skimu hiyo ambayo serikali ilitumia zaidi ya Sh.bilioni 2.1 kuijenga lakini idadi kubwa ya wakulima hawalimi huku wengine wakiyakodisha mashamba kwa watu wengine.

Alisema serikali haiwezi kukubali kuona katika mradi huu ambao serikali ilimewekeza mabilioni ya fedha ekari 40 tu ndizo zonazolimwa kati 209 walizogawiwa wakulima ambao ni wananchama wa umoja wa umwagiliaji Itigi.

"Serikali imewekeza fedha nyingi sana kwenye mradi huu lakini hatujautendea haki na hata maji yanafika hapa lakini hapalimwi, hii haikubaliki lazima watu walime ili kuisaidia Serikali kupata mapato na Tume ya Umwagiliaji nao wapate tozo zao," alisema.

Alisema matumaini ya serikali ni kuona eneo lote linalimwa wakati wa kiangazi na masika ili baada ya hapo ijengwe hoja ya kutaka kuongezewa eneo jingine la kulima.

Kufuatia hali hiyo,Mkuu wa Mkoa alimwagiza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Itigi, Diwani na Mtendaji Kata kuandaa mkutano ili waweze kuwajua watu wasio na  uwezo wa kulima wasikodishe mashamba wapewe wengine wenye uwezo wa kulima.

"Mwezi wa tisa mwenyekiti andaa mkutano na wanachama wako ili tuje tujue nani analima na nani halimi ili wale ambao hawalimi tuwaondolee mashamba tuwape wengine ambao watalima na kuipa Serikali mapato pamoja na Tume ya umwagiliaji," alisema.

Serukamba alisema wakulima lazima watambue kuwa faida atakayoipata mkulima kupitia kilimo kwenye skimu hiyo itamrahishia maisha kiuchumi ataweza kuhudumia familia, kulipa bima ya afya  pamoja na kuchangia maendeleo ya taifa lake.

"Kuna watu kule Dodoma hawana maji na wangetamani kulima lakini nyie mumepata maji lakini hamtaki kulima hatueleweki unayetaka kulima vitunguu,mahindi mpunga lima," alisema.

Serukamba alisema serikali imetoa mbolea ya ruzuku ambayo sasa itakuwa imauzwa Sh.70,000 hivyo wakulima wajifunze na matumizi ya mbolea katika kilimo hicho.

Mkulima katika skimu hiyo,  Chacha Marwa alisema changamoto  inayokabili wakulima wengi kutolima ni kushindwa kutambua aina ya udongo  pamoja na baadhi ya Wanachama  wa umoja huo wa umwagiliaji waliopewa mashamba kuyakodisha kwa watu wengine.

"Mhe. Mkuu wa Mkoa sisi huu udongo unatuchanganya sana tunashindwa kuelewa tulime mbegu gani tunaomba mtusaidie kutupimia udongo wetu," alisema.

 Chacha alisema kuwa baadhi ya wasimamizi wa skimu hiyo sio waaminifu kwa wanachama wao jambo linalopelekea washindwe kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji kwani wamekuwa wakikodisha mashamba na kuwanyima fursa wengine.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Umwagiliaji Itagata, Stephano Mbonde alisema kuwa mashamba yenye ukubwa wa Ekari 209 yaligawiwa kwa wanachama 321 ambapo ekari 106 ziligawiwa kipindi cha masika.

 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: