Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhani Masumbuko akizungumza wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika leo Jumatatu Agosti 22,2022.

Na Kadama Malunde 
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko ameziagiza taasisi mbalimbali katika Manispaa hiyo kuwa wanapeleka taarifa zao (Makablasha) kwa wakati badala ya kusubiri hadi siku ya kikao na kupeleka taarifa mezani akibainisha kuwa Madiwani hawawezi kusoma makablasha na kuelewa taarifa wakati kikao kinaendelea.

Masumbuko ametoa agizo hilo leo Jumatatu Agosti 22,2022 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

“Nikupongeze Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola kwa kitu kimoja ambacho umekuwa tofauti na taasisi zingine,.... umekuwa wa kwanza kutuletea taarifa yako ambapo Waheshimiwa Madiwani wameipitia vizuri, wakaichakata na wakaielewa na maswali yamepungua. Lakini taasisi zingine tunakutana na taarifa zao mezani, mnategemea sisi tunapata muda gani wa kuelewa mambo haya?, Kablasha la SHUWASA tumelipata mapema sana”,amesema Meya huyo.


“Leteni Makablasha yenu kwa wakati, Sisi siyo mitambo ya kuchakata makablasha wakati kikao kinaendelea…. Sisi siyo mitambo ya kuchakata makablasha kiasi hicho, kwa hiyo tunaomba tuzipokee taarifa hizo mapema, kwa hiyo hili nisisitize hili lisijirudie tena, tulichukue kuwa ni jambo la msingi kwani sisi Madiwani ni wasimamizi wa Halmashauri lazima tuwe na taarifa za kutosha”,amesema Masumbuko.
Share To:

Post A Comment: