Raisa Said,Bumbuli


Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Tanga Husna Sekiboko amesema kuwa takwimu za sensa iliyopita Kwa Wilaya ya Lushoto haikulizisha Kutokana na wananchi Kushindwa kujitokeza Kwa wingi.


Hayo ameyasema Kata ya Vuga, Halmashauri ya Bumbuli wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kujitokeza Kwa wingi kuhesabiwa ifikapo agost 23.


Sekibo alisema kuwa sensa ya mwisho iliyofanyika mwaka 2002 wananchi wa Wilaya ya lushoto walishindwa kujitokeza kwa wingi kushiriki kuhesabiwa Kutokana na Imani potofu huku wakidai jambo hilo linakinzana na dini zote.


"Takwimu zilizoenda sensa iliyopita zilikuwa za uongo sababu nilishuhudia watu wengi walishindwa kushiriki kuhesabiwa kutokana na Imani potofu, sensa ya mwaka huu ni muhimu hivyo agosti 23 jitokezeni kuhesabiwa kwani sensa inatambuliwa na dini zote na sio kinyume kama mnavyosema" amesema  huku akisisitiza wahakikishe wanatoa taarifa za kweli pindi Makarani watakapokuwa wanapita kuchukua taarifa zao..


Mbunge huyo alisema Sensa itawapeleka kwenye namba nzuri yakugawana keki ya Serikali,kipande hiki kiende wapi Kwa ukubwa  upi na hata ili Mkoa uweze kugawanywa ni lazima idadi ya watu itambulike.


Alieleza  kuwa lengo la sensa hiyo ni kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.


Alisisitiza kuwa taarifa  za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali.


Aidha ametoa mfano wa madhebu ya dini kwamba ili dhehebu lijenge nyumba ya kuabudia ikiwa ni msikiti au kanisa ni lazima viongozi wa dini wajue idadi ya waumuni waoShare To:

Post A Comment: