Mbunge  wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, akizungumza na wachezaji wa Timu za Wakala FC, Sokoni FC na waamuzi wa mpira wakati akifungua bonanza la michezo aliloliandaa kwa ajili ya kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022.linaloendelea Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ikungi mkoani Singida ambapo kilele chake kitakuwa kesho.
Mbunge  wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu,  akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa bonaza hilo.
Wachezaji wa Timu ya Wakala FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo dhidi ya Sokoni FC. Katika mchezo huo Sokoni FC ilishinda kwa mabao 4-0.
Wachezaji wa Timu ya Sokoni FC wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mchezo dhidi ya Wakala  FC. Katika mchezo huo Sokoni FC ilishinda kwa mabao 4-0.
Mbunge Mtaturu akifuatilia mchezo dhidi ya Wakala FC na Sokoni FC.
Washariki wakifuatilia mchezo huo.
Mbunge Mtaturu akizungumza na wachezaji wa Timu ya Sokoni wakati akiikagua timu hiyo kabla ya mchezo wao dhidhi ya Wakala FC.
Mbunge Mtaturu akisalimiana na waamuzi wa mchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo wakiwa tayari kwa kazi.Kutoka kulia ni Rehema Dafi, Emanuel Safari na Enock Ayubu.
Mashabiki wakifuatilia mchezo huo. Wa pili kushoto ni Mtangazaji wa mchezo huo, Robert Onesmo kutoka Radio Standard FM ya Mkoa wa Singida.
Washiriki wakiendelea kushuhudia mchezo.
Mwamuzi wa pembeni wa mchezo huoRehema Dafi akiwajibika.
Gari la Matangazo ya moja kwa moja ya mchezo huo likiwa Uwanjani hapo.
Mchezo ukiendelea.
Mchezaji wa Timu ya Sokoni FC,  Kelvin Raphael  (Kushoto) akimenyana vikali na Mchezaji wa Timu ya Wakala FC, Sharifu Juma.
Mtifuano mkali ukiendelea katika mchezo huo.
Kipa wa Timu ya Wakala FC, Melkidezeck Digeya (kushoto) akiokoa moja ya hatari katika lango lake.
Mchezaji Yasin Ibrahi kutoka timu ya Sokoni FC, akijaribu kumtoka mchezaji wa Timu ya Wakala FC.
Kipa wa Timu ya Wakala FC, Melkidezeck Digeya  akiwa amekaa chini huku akishindwa kuamini baada ya timu yake kubugizwa magori manne kwa nunge.

 Wachezaji wa Timu ya Sokoni FC wakishangilia baada ya kuwabugiza wenzao wa Timu ya Wakala mabao manne kwa nunge.


 

Na Dotto Mwaibale, Singida

MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ameunga jitihada za Rais Samia Suruhu Hassan za kuhimiza wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuandaa bonaza la michezo ya aina mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha zoezi hilo.

Akizungumza wakati akifungua bonanza hilo linalofanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ikungi alisema limelenga kuunga jitihada za Rais Samia za kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ambalo ni muhimu kwa Taifa.

“Lengo la bonanza ili ni kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Ikungi  kujitokeza kwa wingi katika zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika Agosti  23, 2022 ili waweze kuhesabiwa kwa maendeleo ya taifa na ili serikali iweze kutupangia mipango mbalimbali ya maendeleo ni lazima tujitojeze kwa wingi kuhesabiwa bila kukosa ” alisema Mtaturu.

Akizungumzia Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Mtaturu alisema ni  pamoja na kuisadia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

Alisema taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali na kupata taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote.

Aidha Mtaturu alisema umuhimu wa sensa hiyo ni pamoja na kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi.

Pia alisema umuhimu wa sensa hiyo ni kupata taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira na msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia.

Alisema bonaza hilo ambalo limeanza leo limeanza kwa mashindano ya timu nne za mpira wa miguu ambazo jumla yake zitakuwa nane na kuwa kesho itakuwa ni kilele cha bonanza  hilo ambapo kutakuwa na michezo ya aina tofauti kama, mchezo wa bao, kuruka kamba kwa akina mama ‘malede’ mchezo wa bao, karata, Netball, kuruka kamba na mingine mingi na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro.

Alizitaja timu zitakazoshiriki bonanza hilo kuwa ni Wakala FC, Sokoni FC, Bodaboda FC, Golden Boys, Matongo FC, Choda FC, Mampando FC na Makiungu FC.

Alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza kwa mpira wa miguu kuwa ni Sh.300,000, mshindi wa pili 200,000 na mshindi wa tatu ataondoka na kitita cha Sh.100,000.

Mtaturu alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki bonanza hilo la kuhamasisha zoezi kujitokeza kwa wingi na kufanikisha zoez la sensa ya watu na makazi 2022.Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: