Na Fredy Mgunda, Iringa.


Baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wameikataa taarifa ya mwaka kutoka kutokuwa imekamilika vilivyo kwa kuwa na upungufu wa baadhi ya taarifa kutokuwepo kwenye taarifa hiyo.


Akizungumza wakati wa kuharisha kikao cha mabaraza la madiwani la mwaka 2021/2022, Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa madiwani wamesema kuwa hawajaridhishwa na taarifa ambayo imetolewa ambayo ilikuwa haijakamilika.


Alisema kuwa taarifa iliyotolewa ya mwaka ilikuwa haijamilika na baadhi ya taarifa ya hazijawekwa kwenye taarifa hivyo wametoa muda kwa waataalam wa Halmashauri kukamilisha taarifa na kuitisha baraza tena.


Meya Ngwada alisema kuwa kamati ya fedha inatakiwa kufanya kazi kwa ufasa kabisa ili kuondoa dosari ambazo zimejitokeza."Mimi ndio mwenyekiti wa kamati ya fedha Mimi ndio kiongozi lakini inatakiwa kamati nzima kujibia maana tupo wengi mzigo huu sio wa meya pekee yangu bali wote inatakiwa kujibu maswala kukosolewa kama ambavyo inatakiwa hivyo hili ni kosa letu wote"alisema Meya Ngwada


Meya Ngwada alisema kuwa Baraza lijalo linatakiwa kuwa na taarifa zote zilizo kamilika ili kuondoa dosari ambazo zimejitokeza kwenye baraza.


Awali kulifanyika uchaguzi wa naibu Meya ambapo diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani alichaguliwa kuwa naibu meya wa Manispaa ya Iringa kwa kuchukua nafasi ya likotiko katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.


Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa naibu meya,Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada alisema kuwa jumla ya kura 26 zilipigwa na hakuna kura iliyoharibika wala hapana hivyo Jully Sawani amechaguliwa kwa jumla ya kura 26.

Share To:

Post A Comment: