Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Injinia Richard Ruyungo ameipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kuwa na bunifu zilizolenga kutatua changamoto za wakulima na wafugaji .Pongezi hizo zimetolewa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Injinia Richard Ruyungo alipotembelea banda la Taasisi hilo Agosti 3, 2022 wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 28 ya nanenane kanda ya Kaskazini viwanja vya Themi Arusha.

Injinia Ruyungo amesema kuwa bunifu ya mbolea asilia yotokanayo na vimelea vya bakteria jamii ya rhizobia ambayo inasaidia kuongeza virutubisho vya nitrogeni na fosforasi kwa mimea ya Soya ni kwa muhimu kwa wakulima wa zao la Soya.

"Hongereni kwa bunifu hizi nzuri zilizolenga kuwakomboa wakulima, naomba zisiishie tu kwenye maonyesha bali ziwafikie walengwa hususani wakulima wa vijijini" amesema Injinia Ruyungo 


Anazidi kueleza kuwa huduma ya upimaji wa udongo inayotolewa na taasisi hiyo ni muhimu sana kwa wakulima kwa kuwa inawasaidia kujua aina ya udongo na hivyo kujua zao linaloendana na huo undogo hivyo kuongeza uzalishaji katika mazoa.

Naye Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afrika Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Dr. Ernest Mbega ametoa rai kwa wabunifu hao hususani wa migomba iliyoboreshwa kuzalisha migomba yenye ubora ili kuongeza mapato ya chuo.

"Teknolojia hii ya kuboresha migomba iliyoboreshwa ni chanzo kizuri cha mapato kwa taasisi , tuzalishe zao hili kwa wingi ili kupata soko zuri" amesema Dr. Mbega

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imeshiriki maonesho ya 28 ya nane nane kanda ya Kaskazini kwa kuonyesha bunifu na tenolojia ambazo zimelenga kutatua changamoto mbalimbali zinzowakabili wakulima na wafugaji.

Bunifu na Teknolojia hizo ni pamoja na jiko maalum la kupikia ugali " Ugali Smart Cooker" ,migomba iliyoboreshwa,kiatilifu biologia cha kudhibiti wadudu katika zao la Kabeji, upimaji wa udongo, chakula cha samaki chenye lishe, buheri wa Afya, Nutrano, NUSA, Omega -3DHA,Ngwara,Tunda la kweme na yakula vya asili visivyo na kemikali.
Share To:

Post A Comment: