Na Joel Maduka Geita. 


Wananchi wa  Wilaya ya Chato na  maeneo jirani ya  mkoa wa Geita wamehimzwa kuendelea kujitokeza  kupatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kanda Chato kwani kwa sasa hospitali hiyo inavifaa vya kutosha na inatoa huduma zakibingwa kwa magonjwa yote.


Wito huo na Mkuu wa wilaya ya Chato Martha Mkupasi mapema  leo kwenye ufunguzi wa juma la maadhimisho ya   mwaka mmoja wa utoaji huduma ya Hospitali hiyo ambayo ilianza kutoa huduma za rufaa tarehe 30 Julai 2021.


Mkuu wa Wilaya amesema kwa sasa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato imepokea vifaa vingi hivyo ni vyema jamii ikaelewa kuwa hospitali hiyo ipo tayari kupokea wagonjwa wa aina yoyotekutoka maeneo ya karibu na mkoa wa Geita. 


“Kwa sasa hospitali ina wataalamu wengi waliobobea, ina vifaa vingi na vizuri leo tumejionea wenyewe ndani ya hospitali hii, ni Imani yangu wagonjwa watatibiwa vizuri na kwa wakati”amesema Mkuu wa Wilaya ya Chato.



Mbunge  wa jimbo   la Chato  Dkt.Medard  Kalemani  ameishukuru  serikali  ya  awamu  ya sita kuendelea kutoa fedha kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo ambapo amesema kukamilika kwahospitali hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato imesaidia wananchi wa Chato na mkoa wa Geita kwa ujumla kupatiwa matibabu kwa gharama nafuu na haraka kwani hapo awali walilazimika kwenda Mwanza kwa ajili ya matibabu.


“Mheshimiwa Rais atembee kifua mbele, fedha anazoleta tunaona zinafanya kazi nzuri, na sisitunamhakikishia   tutalinda   miundombinu   ya   hospitali   hii   kwani   matunda   yake   tunayaona”amesema Mhe. Dkt. Medard Kalemani


Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Dkt. Oswald Lyapa amesema hospitali hiyoimeweza kuhudumia   wagonjwa 10,502 tangu   ianze kutoahuduma   tarehe 30 Julai   2021.



Amesema wagonjwa wengi wanaopatiwa huduma wanatoka mikoa ya Geita, Kagera, Kigoma naShinyanga.


Hospitali ya Rufaa  ya Kanda ya Chato ilianza kujengwa mwaka  2017  na inakadiriwa kutoahuduma kwa wagonjwa 700 hadi 1000 kwa siku. Kwa sasa hospitali hiyo inatoa huduma zakibingwa za upasuaji, huduma za mama na mtoto, magonjwa ya ndani, huduma za utoaji dawana vifaa tiba, huduma za uchunguzi wa afya na huduma za mionzi.


Hadi sasa ujenzi wa hospitali hiyo umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 25 ambapo kwa sasa serikali kupitia fedha za UVIKO 19 imetenga shilingi bilioni 6 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tibaikiwa ni pamoja na CT Scan, MRI,X-Ray pamoja na vifaa vya wagonjwa mahututi na wagonjwa wa dharula.



Share To:

JUSLINE

Post A Comment: