Na John Mhala,Longido

 

Naibu Waziri wa Madini,Dkt Stephen Kiruswa jana alikabidhi tani 200 ya Mahindi katika Vijiji viwili vya Olmolog na Elerai vilivyopo katika Wilayani Longido Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwapooza na uhaba wa chakula unaowakabili baada ya mifugo yao kutaifishwa.

Dkt Kiruswa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Longido alisema wananchi hao walikiuka taratibu zilizowekwa na  serikali kwa kuvamia shamba la Mwekezaji anayemiliki shamba la Mount Saad Farm lakini viongozi wa serikali wa wilaya ya Longido na Siha walikubaliana kumaliza kesi nje ya Mahakama lakini viongozi wa Siha waligeuka makubaliano.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassaan aliwahi kusema katika hotuba zake kuwa sheria iko na inapaswa kutekelezwa lakini kama busara inaweza kutumika kwa ajili ya wananchi hilo linapaswa kufanyika kwa ajili ya manufaa ya pande zote lakini hilo halikufanyika kwa kuwa viongozi wa Siha wakiuka makubaliana kwa makusudi kitu ambacho sio sawa.

Mbunge huyo alisema mifugo Zaidi ya 1,300 ilitaifishwa na kuwaacha wananchi wakiwa masikini na ukizingatia kuwa kipindi hiki ni cha ukame na kutoka na hali hiyo serikali imeamua kutoa tani 200 yenye magunia 600 kwa ajili ya kupooza njaa kwa wananchi hao.

‘’Sheria ipo na inapaswa kutekelezwa ila kama kuna umuhimu wa kukaa na kukubaliana nje ya Mahakama kwa kutumia busara hilo linapaswa kufanyika kama serikali ilivyoamua kutumia busara na kuwapelekea wafugaji hao mahindi’’ alisema Mbunge

Katika kuwasaaidia wananchi hao,Dkt Kiruswa naye alikabidhi kiasi cha Tani moja kwa wananchi wa Vijiji hivyo kwa lengo la kwasaidia katika kipindi hiki kigumu kinachowakabili kwa sasa.

Diwani kwa kata ya Olmolog,Loomoni Ole Siato Pamoja na kumshukuru Mbunge na serikali kwa msaada huo ila amesikitishwa sana na viongozi wa serikali ya wilaya ya Siha kwa kufanya maamuzi yenye kuijenga chuki kati ya serikali na wananchi wakati jambo hilo lilipaswa kumalizwa nje ya Mahakama.

Alisema Mahakama iko kwa ajili ya kutekeleza sheria dhidi ya wale wanaokiuka taratibu na kama jamba linaweza kuzungumzwa nje ya Mahakama kwa lengo la kuleta amani kati ya serikali na jamii ni vema busara ikafanyika ili kila mmoja aweze kufanya jukumu lake kwa amani na upendo.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Elerai,Samoni Ole Sailalei alisema kuwa jamii yote ya vijiji hivyo iko katika hali mbaya ya uhaba wa chakula na uamuzi wa serikali na Mbunge kutoa msaada wa chakula kwa wananchi hao ni jambo linalopaswa kushukuriwa kwa kuwa serikali imeona wazi kuwa busara hakutumika katika maamuzi ya jambo hilo.

Sailalei alisema wananchi wa vijiji hivyo kwa sasa wanaishi Maisha magumu sana baada ya mifogo yao yote kutaifishwa kwani miezi hii katika vijiji hivyo kuna ukame na kufuatia msaada huo hali inaweza kuwa tofauti kwa sasa.


Alisema na kushangazwa kuwa wananchi wa Siha mifugo yao inalishwa katika ardhi ya wilaya ya Longido lakini kufuatia uhusiano mzuri waliokuwa nao hawaweze kulipiza kisasi kama walivyofanya wao.


 










 


Share To:

Post A Comment: