Wakulima wa shayiri katika mikoa ya Arusha na Manyara wamesema kwa mwaka 2022 wameingia katika madeni makubwa kutokana na kupata hasara kwenye kilimo hicho, iliyochangiwa na uhaba wa mvua uliosababishwa na Athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.


Mikoa hiyo ina Wakulima  mia tatu na arobaini na saba wanaolima kilimo cha mkataba na kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) wameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya wakulima wa shayiri ambayo yamefanyika katika mashamba yao yaliyopo wilayani Monduli mkoani Arusha.


“Mabadiliko ya tabia ya nchi  kwa mwaka huu tuseme yameathiri kwa asilimia 99.5, wakulima Mbegu tulipata kwa wakati, pia tumelima kulingana na kanun izote za kilimo lakini kwa sasabu ya sisi tunalima kwa hali ya hew ana sio umwagiliaji, kwa kweli imetuathiri na hakuna chochete tunatazamia kwenda kukivuna” Alisema Bi Einot Solomon, Mkulima wa shahiri Arusha.


Hata hivyo wakulima hao wameiomba serikali Pamoja na wadau wengine hasa walioingia nao mkataba Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL)  kuangalia namna ya kuwasaidia ili kujikwamu kwenye hali hiyo.


‘’Tunatamani na wao waweze kutufikiria, wadau walitupa mbegu na tunatakiwa kuzilipa pale tupakapopeleka mazao ya kwetu kuwauzia, sasa watuangali maana hakuna chochote tutakachokipeleka mwaka huu, waangalie namna ya kutusamehe mbegu walizotupa mwaka huu’’  Durisho Duru Mkulima wa Shahiri.


Kwa upande wao wa uongozi wa Kampuni ya uzalishaji wa bia Tanzania (TBL) kupitia kwa Meneja Kilimo Joel Msechu alikiri wakulima hao kupata hasara yaliyosababishwa na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na kueleza kuwa wamekuja na mkakati wa kuwaunganisha na makampuni ya bima ili kuwawesha huduma hiyo itakayowasaidia kuwakinga na majanga ikiwemo ukame.


Hata hivyo Joel ameongeza Kwa kusema kuwa TBL itaendelea kuwapatia masoko ya uhakika ya mazao yao na vilevile kuwapatia ujuzi utaowawezesha kufanya kilimo cha kisasa na endelevu kitakachowawezesha kuongeza mchango wa sekta ya kilimo kwenye uchumi wa nchi kama ilivyoidhinishwa kwenye kampeni ya kilimo ya Ajenda 10/30 ya mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.


“Kuwawezesha wakulima wadogo ni moja ya ahadi xa AB InBev kama kama sehemu ya kutimiza malengo endelevu mwaka 2025 ambayo yanaafikiana na maelengo endelevu yam waka 2025 ya umoja wa mataifa (SDG) alisema Msechu


Maadhimishi hayo siku ya wakulima wa shayiri yanalenga kuongeza ari ya kuboresha mnyororo wa thamani kwenye kilimo.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: