Muwakilishi wa Mkuu wa Ofisi ya UNESCO, Bw. Mathias Luhanya akimkabidhi Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Amon Mpanju nakala za madaftari ya kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia katika uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha Dodoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Amon Mpanju akipokea nakala za madaftari ya kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia katika uzinduzi wa dawati la Jinsia la Chuo Kikuu cha DodomaKutoka kushoto, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Faustine Bee, Muwakilishi wa mkuu wa ofisi ya UNESCO Bw. Mathias Luhanya,Mgeni rasmi Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe, Dr. Lilian Makalanga, mratibu wa kitengo cha Jinsia Chuo kikuu cha Dodoma, kwa pamoja wakikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa dawati.

**********************

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, kwa kupitia programu yake ya “Our rights, Our Lives, Our future Plus” inayofahamika kama O3 Plus imekabidhi nakala 800 za madaftari ya kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia kwa serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi maalum katika uzinduzi wa dawati la jinsia la chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).

UNESCO katika kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kama moja ya lengo la maendeleo endelevu inashirikiana na wadau wa elimu kuweka mazingira salama na jumuishi ya kusomea kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu na elimu ya kati wa Tanzania, ili kufanikisha wanafunzi kumaliza safari yao ya elimu bila vikwazo.

UNESCO inaunga mkono juhudi za serikali kwenye kuanzisha na kuendesha shughuli za dawati la jinsia katika taasisi za elimu ya juu na elimu ya kati, imeshirikiana na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma kawenye ufunguzi wa dawati la Jinsia na kukabidhi madaftari ya usajili wa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia .ambapo lengo lake ni kusajili na kutunza kumbukumbu za taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotolewa katika Dawati la Jinsia chuoni hapo.

Kwa kupitia mradi wa O3 Plus unaofadhiliwa na serikali ya Sweden UNESCO imechapisha nakala 800 za madaftari ya kusajili Umuhimu wa daftari la kusajili taarifa za ukatili wa kijinsia ni Pamoja na:
i) Kuwezesha ufuatiliaji wa mwenendo wa shauri lililopewa rufaa; ii) Kusaidia kuongeza wigo wa kupata taarifa za vitendo vya ukatili; na

iii) Kuwezesha uandaaji wa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia zilizoripotiwa katika Dawati

UNESCO inalenga kuongeza uelewa wa wadau zaidi ya 50,000 wa vyuo vikuu kuhusu ukatili wa kijinsia na vitendo vya unyanyasaji wa kingono, kutoa samani za ofisi kwa ofisi za madawati 10 ya jinsia ya vyuo vikuu, kutoa mafunzo kwa waratibu wa madawati ya jinsia wapatao 200 kutoka vyuo vikuu 15, na kuwezesha usambazaji wa nakala za vitabu vya rejista ya dawati la jinsia kwa mradi wote wa vyuo vikuu nufaika.

Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: