Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dkt.Mashimba Ndaki akifungua Mkutano wa SADC uanaolenga kuongeza mnyororo wa thamani wa nyama nyekundu inayotokana na Ng'ombe wa asili unaofanyika kwa siku 7 Jijini Arusha 
Waziri Dkt.Ndaki akipokea Zawadi kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Muungano wa Afrika wa Rasilimali za wanyama Dkt. Nick Mwankpa katika mkutano huo picha zote na Moses Mashalla 

Na Moses Mashalla


Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Mashamba Ndaki ameeleza kwamba katika kipindi cha miezi sita Tanzania imeuza nyama tani elfu 10 katika nchi za Bara la Asia tofauti na miaka ya nyuma na huenda Mwaka huu ikauza zaidi ya miaka yote. 

Ndaki ameyasema hayo jijini Arusha  wakati ya akifungua warsha ya siku saba ya wataalamu wa sekta ya mifugo kutoka  nchi za  jumuiya  ya maendeleo kusini mwa Afrika{SADC}  unaolenga kujadili namna ya kuongeza thamani ya nyama nyekundu yanayotokana na ng’ombe wa asili.


Amesema  kuwa, ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika nchini za Bara la Asia hususani nchi za kiarabu imeweza kufungua mwanga kwa nchi hizo kuwa wanunuzi wakubwa wa nyama ya hapa nchini na hadi kufikia Desemba mwaka huu huenda Tanzania ikauza nyama nyingi kuliko miaka yote.

 

Waziri Ndaki  amesema  kuwa,kutokana na hilo kupitia Wizara yake wamepanga mpango kazi wa kuhakikisha wanafuga mifugo bora yenye lengo la kumpatia mlaji bidhaa bora kwa maslahi ya nchi.

 

“katika kipindi cha mwaka mzima wa mwaka jana Tanzania iliuza nje ya nchi nyama tani Elfu 7 lakini kwa mwaka huu hali imekuwa tofauti sana kwani katika kipindi cha miezi sita nchi imefanikiwa kuuza nje ya nchi nyama ya kiasi cha tani Elfu 10.”amesema Waziri Ndaki.


Waziri amesema kuwa, kutokana na hali hiyo Wizara  imepanga kuboresha sekta ya Mifugo kwa kufuga kisasa katika vituo vyake vya ng’ombe na mbuzi kuwa na mifugo yenye ubora itakayoshindana na soko na huku akiwataka wafugaji kufanya hivyo kwa maslahi ya nchi.

 

Amesema  kuwa, katika kuboresha hilo Wizara imepanga kujenga mabwawa ya Mifugo zaidi katika Mikoa yote yenye mifugo mingi, pamoja na kujenga majosho kwa ajili ya kulinda ugonjwa kwa mifugo.

 

Waziri Mashimba ameongeza  kuwa serikali imepanga kushirikiana na nchi za SADC katika kuboresha mifugo na kuwa na nyama bora kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi kwani nchi za SADC zina mifugo bora kuliko nchini zingine katika Bara la Afrika.


Mtaalamu wa maswala ya teknolojia ,ujuzi na ubunifu katika mradi wa Live2Afrika (AU-IBAR)Dk Mary Kariuki amesema kuwa,wamekuwa na mijadala ya kutosha katika eneo hilo katika kuhakikisha wanaboresha mnyororo wa nyama wa thamani katika eneo la kimazingira katika nchi za ukanda wa SADC.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Muungano wa Afrika kwa rasilimali za Wanyama(AU -IBAR) Dk .Nick Mwankpa amesema kuwa, wataalamu wa nchi hizo watatoka na maazimio yenye tija kwa nchi hizo na kwenda kufanyiwa kazi kwa ajili ya faida ya nchi hizo na sio vinginevyo.

 Dk Mwankpa alisisitiza kuwa Lengo la warsha hiyo ni kuongeza thamani ya mazao ya mifugo barani Afrika ili wafugaji waweze kunufaika na Rasilimali zao na kuondoa Utamaduni wa kumiliki mifugo mingi pasipo  kuwa na faida. 

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: